Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 8 April 2015

BABA YAKE MKUDE AZIKWA JIJINI DAR


Mkude akiwa ameshikilia msalaba wa baba yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar leo jioni.

Mkude akiweka shada la maua baada ya mazishi ya baba yake katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiweka shada ya maua katika kaburi la mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude, leo jijini Dar.

Kiungo wa Simba, Abdi Banda (wa pili kushoto) akiwa na waombolezaji wengine katika msiba wa mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo mwenzake wa Simba, Jonas Mkude.

Kiungo wa Simba Jonas Mkude akiwa na majonzi wakati akisikiliza misa ya ibada katika msiba wa baba yake mzee Gerald Mkude, Konondoni jijini Dar.

Makamu wa Rais wa Simba, Kaburu akimfariji Jonas Mkude katika msiba wa baba yake, nyumbani kwao, Kinondoni Studio jijini Dar.

Viongozi wa Simba, kutoka kushoto: Frisch Colins, Kaburu na Ally Suru wakiwa katika Makaburi ya Kinondoni kufuatilia mazishi ya baba mzazi wa kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude.

MZEE Gerald Jonas Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amezikwa jana Jumanne jioni katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo tangu Novemba mwaka jana.

Mzee huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 46, alilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala tangu Alhamisi ya wiki iliyopita kabla ya Jumapili kufariki akiwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni.
Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lihimidiwe, amina.

CREDIT: GPL

No comments:

Post a Comment