Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 12 August 2014

VIJIJI 80 KUNUFAIKA NA UMEME WA REA UTAKAOGHARIMU SHS. 40 BILIONI

Umeme-jua vijijini

Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: ZAIDI ya vijiji 80 katika wilaya za longido na arumeru vinatarajia kunufaika na mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA) utakaogharimu kiasi cha Shs. 40 bilioni.
Aidha hadi ifikapo Julai 2015 vijiji hivyo vyote vilivyopo katika wilaya hizo vitakuwa vimeshaunganishiwa umeme wa  mradi huo ambao tayari umeshaanza kutekelezeka kwa maeneo mbali mbali  lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi walioko vijijijni kunufaika na nishati ya umeme kwa gharama nafuu.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa kampuni ya  East Africa Electrical Power Solution iliyoko chini ya wakala wa usambazaji umeme vijijini Mhandisi Werema Joseph alipokuwa akizindua rasmi uwekaji wa nguzo za mradi huo katika kijiji cha kiserian kilichopo Mlangarini wilayani Arumeru.
Aidha mhandisi huyo amedai kuwa hadi ifikapo july 2015 watahakikisha kuwa wananchi wote walioko vijijini katika wilaya hizo mbili watakuwa wamenufaika na mradi huo ambao umelenga kuwakomboa kwa kiwango kikubwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao wanakabiliwa na swala la nishati ya umeme.
Alifafanua kuwa ili kuhakikisha kuwa mradi huo unawafikia walengwa kwa haraka  hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu vijiji 20 vitakuwa tayari vimeshanufaika na umeme huo.
“Kwa sasa tumeshaanza kutekeleza mradi huu longido na arumeru na tayari nguzo za kutosha zipo na zoezi hili tunalipeleka kwa haraka kwani kwa wiki tuanatarajia kuweka  kilomita nne tuzimalize ili tuweze kuwasogezea wananchi hawa huduma kwa karibu zaidi,” aliongeza Werema.
Aidha akielezea changamoto zinazowakabili katika mradi huo kuwa ni pamoja na wananchi kulalamika kuhusiana na mashimo yaliyochimbwa na kukaa kwa muda bila kufukiwa kwa nguzo jambo ambalo linawafanya kufanya kazi zaidi.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuwa wavumilivu na hayo mashimo kwa kuwa hatua za kwanza zimeshakamilika na kwamba watapata umeme kwa muda mfupi.
Nae kaimu fundi mkuu wa tanesco arusha mhandisi Beatus Rwegoshora alisema kuwa mradi huo wa kiserian utasaidia maeneo mengi hasa mashule,zahanati pamoja na wananchi na kuwataka kufanya maandalizi ya kuunganishiwa umeme huo kwa kuwa ni mradi wa uhakika zaidi.

No comments:

Post a Comment