Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 12 August 2014

SIYO TANZANIA TU, HATA MAREKANI POLISI WAUA RAIA KWA RISASI!

Waombolezaji wakitoa heshima zao eneo ambalo Michael Brown aliuawa.
Kwa siku ya pili mfululizo kumekuwa na mapambano katika Mji wa Missouri nchini Marekani kufuatia kifo cha kijana mmoja mweusi, Michael Brown, ambaye alipigwa risasi na polisi katika Kitongoji cha St Louis siku ya Jumamosi.
Mkuu wa polisi wa kitongoji cha watu weusi cha Ferguson, Tom Jackson amesema kwamba polisi walitumia gesi na risasi za bandia ili kuwatawanya watu waliokuwa wamefurika karibu na jengo ambalo liliteketezwa kwa moto siku ya tukio ambapo maduka yaliporwa bidhaa na magari yaliharibiwa vibaya.
Ni wakati huo wa utumiaji wa gesi na risasi bandia ndipo raia walipoamua kuwarushia mawe polisi,polisi nao wakajibu mapigo kwa kuwarushia risasi raia hao.

Kijana Michael Brown,alipigwa risasi kadhaa alipokuwa amening'inia kwenye gari ya polisi, na kufuatia tukio hilo FBI wanachunguza endapo kuna uvunjifu wa haki za binadamu katika tukio hilo la kuuawa kwa kijana Michael Brown.
BBC

No comments:

Post a Comment