Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 12 August 2014

SEMINA YA UTHAMINISHAJI MADINI KUFANYIKA BAGAMOYO

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) inatarajia kufanya semina ya siku mbili ambayo itahusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda na Afisa Madini Wakazi yenye lengo la kujadili utendaji kazi, mafanikio pamoja na maboresho ya tasnia ya vito na almasi nchini.
Semina hiyo itakayofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, inatarajiwa kuanza Agosti 14, 2014 na kumalizika Agosti 15, 2014.
TANSORT itaendesha semina hiyo ili kuboresha shughuli za uthamini wa almasi na madini ya vito kwa lengo la kukokotoa mrabaha, kutayarisha miongozo ya bei za madini zinazotumika kukokotoa mrabaha, kutoa huduma za kijemolojia (Gemological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kusimamia mauzo ya almasi na madini ya vito ndani na nje ya nchi.
Semina hiyo itawawezesha washiriki kutoa maoni yatakayowezesha Kitengo hicho kuboresha huduma za kutoa ushauri wa masoko, ukataji na ukadiriaji thamani kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kufanya utafiti wa masoko na bei za almasi na madini ya vito, kutunza takwimu za uzalishaji na mauzo ya almasi na madini ya vito na kusimamia tasnia ya almasi na madini ya vito nchini.
Kitengo cha TANSORT kilianzishwa mwaka 1966 malengo yake yakiwa ni pamoja na kusimamia mrabaha stahiki unaokusanywa na kulipwa serikalini na kuhakikisha madini ya almasi na vito yanayozalishwa nchini yanapata bei bora.
Imetolewa na: 
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
12 Agosti, 2014

No comments:

Post a Comment