Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 14 August 2014

DK. BILAL AWATAKA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUFIKIRI KUJIAJIRI BADALA YA KUAJIRIWA


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: MAKAMU wa Rais, Dk Gharib Bilal amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuajiriwa badala yake watumie taaluma zao ili waweze kujiajiri wenyewe.
Bilal aliyasema hayo jana Jijini hapa  wakati akifungua kongamano la sita la Tume ya  Elimu ya Vyuo Vikuu (TCU) kwakushirikiana naWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Alisema lengo kuu la jukwaa hilo ni kuangalia changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini katika kuhakikisha zinaopatiwa ufumbuzi ili viweze kufikia viwango vikubwa zaidi katika sekta ya elimu  hapa nchini.
Alisema Tanzania imepiga hatua kubwa katika malengo ya milenia yanayoishia mwaka 2015 lakini sekta ya elimu ni vyema ikapewa kipaumbele zaidi ili kuwezesha wataalam wengi kujikita kwenye taaluma zao.
“Ni lazima tutafutembinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali za elimu ikiwemo wanafunzi kuweza kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa hii itatuongezea ukuzaji wa ajira zaidi”.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu , Profesa Awadh Mawenya alisema kuwa ni vyema kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu ili kuboresha sekta hiyo na kutoa rai kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na tabia ya kusubiri kuajiriwa badala yake wabuni mbinu zitakazowawezesha kupata ajira pindi wamalizapo vyuo.
Pia alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Vyuo Vikuu itaendelea kuchukua  hatua za  kusimamia na kuimarisha ubora wa elimu ya juu nchini ikiwemo kufuatilia mwenendo wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki baada ya kutunukiwa  hati idhini ili viendelee kuzingatia ubora unaokubalika.

No comments:

Post a Comment