Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 20 June 2015

WASANII MAARUFU WA 'MIZENGWE' WASHAMBULIA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Displaying 2.JPG
“UTII WA SHERIA BILA SHURUTI” Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Jesca Kindole (Safina) akilipigia saluti sanamu la askari wa Jeshi la Polisi wa kipindi cha kikoloni, wakati  msanii huyo na wenzake walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Displaying 1.JPG
Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe kinachorushwa na Kituo cha ITV, wakichukua vipeperushi vya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi toka kwa Afisa wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Pendo Mtama (kulia) wakati wasanii hao walipotembelea mabanda ya Wizara hiyo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina).
Displaying 3.JPG
Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, wakipewa maelezo na Koplo wa Jeshi la Polisi, Sylvester Mganga, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku), Jesca Kindole (Safina) na Rashid Costa (Maringo 7).
Displaying 4.JPG
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba (kulia) akiwapa maelezo wasanii maarufu wa vichekesho wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jesca Kindole (Safina) na Habib Mrisho (Sumaku).
Displaying 5.JPG
Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Habib Mrisho (Sumaku) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Jeshi la Magereza wakati msanii huyo na mwenzake Jesca Kindole kwa jina maarufu la uigizaji (Safina -kulia) walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa wa Jeshi hilo.
Displaying 6.JPG
Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaochekesha katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, kutoka kulia Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina) wakisoma Hati za Kusafiria zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji. Wasanii hao walitembelea Mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Idara hiyo, Tatu Burhan. Kutoka kulia ni Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina).

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment