Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini (CGP), John Minja akimkarisha Rais Jakaya Kikwete (kushoto)
katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kwa
ajili ya kufunga mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo.
Maafisa 104 wa kozi hiyo walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia), akimkarisha Rais Jakaya Kikwete kuketi
baada ya kukagua gwaride la wahitimu 104 wa kozi ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi
la Magereza kabla ya Rais huyo kuyafunga mafunzo hayo katika sherehe
iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja,
na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Rais Jakaya Kikwete
akimvisha muhitimu Amina Lidenge, Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la
Magereza kwa niaba ya wenzake 104 waliomaliza mafunzo hayo katika Chuo cha
Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga
mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo baada ya
kuyafunga aliweza kutembelea mabanda na kuonyeshwa bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
Rais Jakaya Kikwete
akikagua gwaride liloandaliwa kwa ajili yake na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi
wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kabla ya kuyafunga mafunzo ya Cheo cha
Mrakibu Msaidizi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi
hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo
yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo alikagua bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
Kikosi cha Gwaride la
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kikipita
mbele ya Jukwaa Kuu kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete (hayupo
pichani) katika sherehe ya ufungaji wa mafunzo hayo ya Cheo cha Mrakibu
Msaidizi yaliyofanyika katika viwanja
vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wahitimu 104
walivishwa cheo hicho. Ufungaji wa mafunzo hayo yalienda sambamba na Siku ya
Magereza ambapo Rais KIkwete alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi
hilo nchini.
Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini (CGP), John Minja akitoa hotuba yake kabla ya Rais Jakaya Kikwete
(hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo
pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo.
Katika hotuba yake CGP Minja alisema jeshi lake linakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ukosefu mkubwa wa nyumba za askari na maafisa Magereza.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi pamoja na kumkaribisha Rais
Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa ajili ya kuzungumza na askari, maafisa wa
Jeshi la Magereza pamoja na wageni waalikwa na baadaye kuyafunga mafunzo ya
Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo cha Mrakibu
Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema
Jeshi hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa magereza.
Rais Jakaya Kikwete
akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza, wageni waalikwa na
wananchi wakati akiyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo na
kuwatunukia vyeo vya Warakibu Wasaidizi 104. Katika hotuba yake Rais Kikwete
aliwapongeza wahitimu hao kwa kutunukiwa vyeo hivyo, na pia aliwataka maafisa
wa Jeshi hilo wafuate sheria kwa wawatendea haki Mahabusu na Wafungwa katika
magereza nchini.
Kikosi Maalumu cha
Ukakamavu cha Jeshi la Magereza (KMKM) kikimuonesha Rais Jakaya Kikwete na
wageni waalikwa (hawapo pichani) jinsi kikosi
hicho kinapokuwa kazini wakati wanapopambana na wahalifu wa aina tofauti. Rais
Kikwete aliyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na
kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe
iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es
Salaam.
Kikosi cha gwaride wa
Askari wa Jeshi la Magereza la zamani (askari jela) likionyesha jinsi kipindi
cha zamani jeshi hilo lilivyokuwa linafanya gwaride lake katika sherehe na
shughuli mbalimbali za Jeshi hilo. Tukio hilo lilifanyika kabla ya Rais Jakaya
Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi
hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo
katika sherehe iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete
(wakumi kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maafisa wa Jeshi la Magereza, wahitimu
pamoja na wageni waalikwa, baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za
Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa
jeshi hilo.
Rais Jakaya Kikwete
akiiangalia bilinganya wakati alipokuwa anatembelea mabanda yenye bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa na Jeshi la Magereza nchini. Rais Kikwete alitembelea
maonyesho hayo maalumu yanayofanyika kila mwaka katika Siku ya Magereza, mara baada
ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na
kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo, katika tukio
lililofanyika Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Afisa Kilimo wa Jeshi hilo, Yesaya
Kitundu. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na
anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment