Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras
Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limepokea mapendekezo mapya kutoka serikali ya Ugiriki yanayojaribu kumaliza tatizo la mgogoro wa kiuchumi nchini humo.
Taarifa zaidi za mapendekezo hayo hazikuwekwa wazi, lakini afisa mmoja mwandamizi kutoka Tume ya Umoja wa Ulaya amesema mapendekezo hayo yana mwelekeo mwema katika mkutano wa dharura utakaofanyika leo huko mjini Brussels.
Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, ameshauriana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mipango hiyo kwa kupitia njia ya simu.
Mhariri wa BBC kuhusu maswala ya Uchumi amesema Ugiriki inaamini kwamba imewasilisha mapendekezo yanayofaa ingawa yanaweza yasifike mbali katika kuridhisha baadhi ya nchi.
Spika wa Bunge la Ugiriki, Zoe Kostantopoulou, amesema wakopeshaji sharti waheshimu matakwa ya watu ambao ni raia wa Ugiriki:
raia wa ugiriki wamefanya maamuzi ya kubadilisha sera tarehe 25 mwezi Januari. Wale wanaotaka kusema kwamba uchaguzi hauna maana hawaitendei haki Ugiriki, Umoja wa Ulaya na demokrasia.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment