Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday 26 June 2015
WAKULIMA TUMBAKU UYUI.WAINGIWA HOFU YA MASOKO
Na Hastin Liumba, UyuiWAKULIMA wa zao la tumbaku wilaya ya Uyui mkoani Tabora wako katika hali ya sintofahamu baada ya kukosa masoko ya kueleweka ya wanunuzi wa tumbaku.
Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Uyui Mussa Ntimizi alisema mpaka sasa wakulima hawaelewi watauza wapi tumbaku yao na lini.
Alisema wananchi wengi wanalalamikia kusuasua kwa masoko ya zao hilo hapa nchini jambo ambalo linawatia hofu kubwa na baadhi yao wameanza kukata tamaa hasa baada ya kusubiri kwa muda mrefu pasipo kupata majibu ya uhakika.
Alifafanua kuwa baadhi ya vyama vya msingi vya wakulima hao vinalalamikia kitendo cha kuambiwa wauze asilimia 20 kwanza kisha wamalizie asilimia 80 iliyobaki, jambo ambalo linawapa wasiwasi na halikubaliki miongoni mwao hata kidogo.
Aidha alibainisha kuwa kuendelea kuchelewa kwa masoko hayo kumeanza kuwaathiri kisaikolojia wakulima walio wengi katika wilaya hiyo na wilaya zingine mkoani humo na hasa ikizingatiwa hilo ndio zao pekee la kibiashara linalowaingizia mapato ya kuwawezesha kuishi na kusomesha watoto.
"Tayari tumemwandikia barua ya kumjulisha hali hiyo Waziri mwenye dhamana ya kilimo na tumemwomba lishughulikiwe haraka ili kuepusha baa la njaa kwa wananchi wetu’, alisema.
Aidha kutokana na hali hiyo alibainisha wazi kuwa kuna baadhi ya maeneo hali si shwari kwani wananchi hawana fedha za kununulia chakula cha kuwatosheleza, hivyo akaomba serikali iliangalie kwa umakini na kulishughulikia mara moja.
Baadhi ya wakulima wa zao hilo walioongea na gazeti hili walionyesha dhahiri kukerwa na kitendo cha kukosa soko la uhakika ambapo waliiomba serikali kuwatafutia masoko ya uhakika na yenye bei nzuri ili zao hilo la kibiashara liwe mkombozi kwa maisha yao kiuchumi na waweze kuwasomesha watoto wao tofauti na hali ilivyo sasa ambapo mnunuzi ndiye anayefaidika zaidi na bei katika soko la kimataifa kuliko mkulima.
Gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) Mkandala Mkandala lakini hakuweza kupatikana baada ya kuambiwa kuwa yuko kwenye kikao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment