Bunge la Ugiriki limeidhinisha kura ya maoni iliyokuwa imetishwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Alexis Tsipras kuhusu mpango wa kuisaidia kiuchumi nchi hiyo uliopendekezwa na wakopeshaji wake.
Akizungumza kabla ya kura hiyo, bwana Tsipras amewataka watu nchini Ugiriki kupiga kura ya hapana kwenye kura ambayo itafanyika tarehe 5 mwezi Julai.
Amewalamu wakopeshaji wa nchi hiyo wakiwemo muungano wa ulaya, benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha duniani kwa kuihangaisha ugiriki.
Amesema kuwa kura ya hapana itaipa ugiriki uwezo wa kufanya majadiliano.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment