Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi,
Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akizungumza na madereva wa taxi wa wilaya ya Ilala(Hawapo pichani) kuhusu kutii sheria za barabarani na kuwasisitiza kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa azungumza jambo na madereva wa taxi wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akijibu maswali ya baadhi ya madereva
Madereva wa Taxi wa wilaya ya Ilala wakiuliza maswali kwa Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa mkutano wao
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akiwaelekeza madereva wa Taxi jinsi yakujiunga na mfuko huo
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akimpa
maelezo mmoja wa madereva wa Taxi wilaya ya Ilala aliyeamua kujiunga na mfuko
wa Peisheni wa PSPF
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akimtolea ufafanuzi kuhusu faida za mfuko wa PSPF wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka(kushoto) akimuonesha mmoja wa madereva ili aweke alama ya dole gumba kwenye fomu za Uchangiaji wa Hiari
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akielezea jinsi ya
ujazaji fomu za Uchangiaji wa Hiari kwa baadhi ya madereva waliovutiwa kujiunga
na mfuko wa Peisheni wa PSPF
Baadhi ya Madreva wa Taxi wilaya ya Ilala wakiendelea kufuatilia kkwenye mkutano wao.
Na Mwandishi Wetu
Madereva taxi katika wilaya ya Ilala jijini dar es salaam
wapokea elimu kutoka kwa mfuko wa pensheni wa PSPF na kuweza kujiunga na mfuko
huo ili kuhakikisha wanawekeza katika mfuko huo kwa manufaa yao hapo baadae
kutokana na kazi zao wanazozifanya kila siku za udereva kuwa ni kazi za kawaida na kuona kuwa Pspf ndio kimbilio kwa madereva hao
Akizungumza wakati wa mkutano huo Afisa
masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua
kuungana na madeeva Tax ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na
kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga
na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia hivyo kama PSPF wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia
Mkuu wa kitengo cha elimu wa jeshi la polisi,kikosi cha
usalama barabarani makao makuu , Abel Swai wakati akitoa elimu ya usalama
barabarani amewaasa madereva wote nchini hususani kwa madereva walio weza
kufika katika mkutano huo wa madereva tax kuweza kuwekeza katika mifuko ya
jamii ni jambo muhimu hasa ukizingatia kwa hali ya sasa maisha kuwa ya kawaida
na uchumi wanchi yetu kuporomoka amewaomba madereva kutumia fursa zinazo tolewa
na mfuko wa pensheni wa PSPF ili wawe na akiba ya mafao yao pindi kazi zinapo
isha na hata kuweza kufaidika na mambo mbalimbali katika mfuko huo
Pia mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam
Josephat Sylvery Tirumanywa amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani
maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati
ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo
kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu iajengwa na sisi
watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza
kuwapa shukrani mfuko wa pensheni wa Pspf kwa hatua ya kuwahamasisha watu
mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananhi
mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.
Miongoni mwa madereva waliohudhuria katika mkutano huo
wameupongeza mfuko wa pesheni wa PSPF
kwa kuweza kuwajali kwa kuwapa elimu juu ya mfuko huo pia wameahidi kushiriki
vilivyo katika kujiunga na mfuko huo ili
kuhakikisha maisha yao yanaenda sambamba na hadhi ya jina na ubora wa
kazi zinazofanywa na PSPF,
”kwani tumeiona fursa kutoka PSPF hivyo hatuna budi
kujiunga na mfuko huu kwani fursa ni kuthubutu,kuhiari, kutendana kuamua na uamuzi tulio uchukua ni kujiunga na PSPF
kwa manufaa ya kwetu pia ya taifa kwa ujumla “pia wawasisitiza kuendelea
kueneza elimu katika mkoa wa dar es salaam wote na hata nje ya mkoa ili watu
watambue fursa zinazo tolewa na PSPF.
No comments:
Post a Comment