Wachezaji wa kigeni wa Yanga, Haruna Niyonzima wa Rwanda (kushoto) na Amisi Tambwe wa Burundi, wakiwa miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaocheza soka la kulipwa Tanzania.
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limepitisha azimio la kila mchezaji wa kigeni kulipa dola 2,000 ( wastani wa Shilingi milioni 5) kwa kila msimu atakaocheza ligi kuu ya Tanzania.
Kiasi hicho cha pesa kitaanza kulipwa katika msimu ujao wa ligi wa 2015/2016 .
Wachezaji wa kigeni waliosalia kuendelea kuchezea timu zao na wale wanaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa.
Msemaji na afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichoketi Jumamosi visiwani Zanzibar ni kuwa kiasi hicho cha pesa kitakuwa ni kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.
Katika miaka ya nyuma, wachezaji wa kigeni kutoka nchi mbalimbali, hasa za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walikuwa hawatozwi kiasi chochote cha pesa licha ya kulipwa mamilioni.
Kizuguto amesema fedha hizo zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu ujulikanao kama (Football Development Fund).
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment