Serikali ya Kenya inasema kuwa watu
watano wanazuiliwa kufuatia shambulizi lililondeshwa na kundi la Al
shabaab kwenye chuo kikuu cha Garissa ambapo karibu watu 150 waliuawa.
Baadhi ya washukiwa hao walikamatwa wakijaribu kutorokea taifa jirani la Somalia,waziri wa usalama nchini Kenya amesema.
Mwanafunzi wa kike ambaye aliponea shambulizi hilo ambaye alipatikana amejificha saa 48 baada ya shambulizi hilo kwa sasa anahudumia na shirika la msalaba mwekundu.
Takriban watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi waliuawa wakati wapiganaji walipovamia chuo kikuu cha Garissa.
Kundi la Alshabaab kufikia sasa limeapa kutekeleza ,mashambulizi mabaya dhidi ya Kenya.
Alshabaab pia lililaumiwa na shambulizi la West Gate mjini Nairobi nchini Kenya mwaka 2013 ambapo watu 67 waliuawa.
Tayari maafisa wa polisi katika taifa jirani la Uganda wanasema wamepokea habari zinazosema kwamba shambulizi kama hilo linapangwa nchini humo.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment