Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 4 April 2015

VPL KUENDELEA LEO JUMAMOSI


Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi wikiendi hii katika viwanja sita nchini, kwa michezo minne kuchezwa leo Jumamosi na michezo miwili kuchezwa kesho Jumapili.


Jumamosi Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es Salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo Mlandizi.

Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya  Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment