Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa katika
picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili kutoka
Uingereza jana.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la
Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa
nyimbo za injili kutoka Uingereza jana.
Kutoka kushoto, Angela Kaonja, Nyakwesy Mujaya na Grace Khuni
Angela Kaonja akimvisha skafu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi, akipokea ua
kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions, Nyakwesy Mujaya,
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
Msama akipeana mkono na Ifeanyi Kelechi,
Msama akiteta jambo na Ifeanyi Kelechi
Ifeanyi Kelechi akiimba moja ya nyimbo zake.
Ifeanyi Kelechi akiimba.
Miller Luwoye.
Anthonia Nwafor.
Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama (wa pili kulia) akiwa na waimbaji kutoka Uingereza.
……………………………………………………………..
NA LOVENESS BERNARD
MWIMBAJI
wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Uingereza, Ifeanyi
Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka
litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Kelechi,
aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jana
saa mbili asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar, akiongozana na wenzake
wanne.
Akizungumza
na waandishi wa habari uwanjani hapo, Kelechi alisema lengo la ujio
wake ni kuhakikisha tamasha hilo linanoga kuliko yaliyowahi kufanyika,
ndio maana amekuja na jopo la waimbaji watano.
“Namshukuru
Mungu kutufikisha salama, nimefurahi sana kufika Tanzania kwa mara ya
kwanza, hasa kuja kuimba kwenye tamasha kubwa kama hili, ambalo naamini
litakuwa chachu ya kumfanya kila mtu kuvutiwa nalo,” alisema.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, alisema
kuzidi kumiminika kwa waimbaji, kunaashiria tamasha hilo litanoga
zaidi.
“Waimbaji
wetu wameshaanza kuwasili nchini na kesho waliobakia
watawasili…Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, tunaisubiria siku
hiyo tu,” alisema Msama.
Tayari
muimbaji Faustine Munishi ‘Malebo’ Mtanzania anayeishi nchini Kenya
tayari kawasili tangu juzi huku Ephraim Sekeleti wa Zambia, Rebecca
Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ kutoka Afrika Kusini watafuata.
Mbali
na waimbaji hao kutoka nje, watakuwepo pia wakali wa hapa nchini
wakiwamo Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro na
wengineo.
No comments:
Post a Comment