Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 14 April 2015

MABINTI WA CHIBOK BADO HAWAJULIKANI WALIKO

Wasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram

Rais anayeondoka madarakani nchini Nigeria Goodluck Jonathan, amesema amesikitishwa kuwa siasa zilipewa kipaumbele kuliko maslahi ya wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka shule moja kwenye mji wa Chibok katika Jimbo la Borno.

Rais Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita watapatikana wakiwa salama
Msemaji wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls (Aisha Yesufu) aliiambia BBC kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa.
Lakini rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzai kinachosimamia jimbo na Borno kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.
Siku ya Jumatatu mkazi mmoja wa mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Gwoza alisema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka kwenye nyumba moja kubwa karibu na nyumba yake.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment