Kikosi cha Yanga
Na Faustine Feliciane
Licha ya kufungwa 1-0 na Platinum ya Zimbabwe katika mchezo wa marudiano jana, Yanga imekabiza mechi nne kabla ya kukamilisha ndoto ya kocha Hans van der Pluijim ya ya kucheza hatua ya ligi ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika.
Kwa kipigo hicho, Yanga imesonga mbele kwa jumla ya magoli 5-2
hatahivyo hivyo kuingia hatua ya timu 16 bora ya Kombe la Shirikisho.
Endapo itavuka raundi ya pili, Yanga itakuwa na kizingiti cha moja
ya timu nane zitakazotolewa katika raundi ya tatu ya Ligi ya Klabu
Bingwa Afrika kwa ajili ya kuingia robo-fainali ya Kombe la Shirikisho,
katikati ya mwaka.
Bao la wenyeji Platinum katika mchezo wa jana uliokuwa ukirushwa na
televesheni ya Azam lilifungwa katika dakika ya 23 mjini Zvishavane.
Timu hiyo ililala 5-1 katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa
wiki mbili zilizopita.
Baada ya kuonyesha makosa madogomadogo katika dakika 45 za kwanza,
Yanga ilirudi uwanjani ikiwa timu tofauti kipindi cha pili na kucheza
soka safi kwa muda mwingi wa robo mbili za mwisho wa mchezo.
Na ingeweza kurudi nyumbani na matokeo ya japo sare kama Haruna Niyonzima asingepoteza nafasi nzuri katika kipindi hicho.
Akiwa ameingia ndani ya eneo la hatari, na akiwa ameshampiga chenga
beki mmoja wa Platinum, Niyonzima alipiga shuti lililokwendan je ya
lango la wenyeji.
Kusonga mbele kwa Yanga ni hatua moja zaidi kuliko mwaka jana
ilipotolewa na Al Ahly ya Misri katika raundi ya kwanza ya michuano
mikubwa zaidi ya ngazi ya klabu Afrika.
Timu hizo zilishinda 1-0 kila moja nyumbani kabla ya Yanga kuaga kwa mikwaju ya penalti jijini Cairo.
Baada ya mafanikio hayo katika anga ya kimataifa, akili ya Yanga
inarudi kwenye ligi kuu ya Bara haraka ambako timu hiyo itakuwa mwenyeji
wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa Jumatano.
Yanga (40) inaongoza ligi kuu ya Bara kwa tofauti ya pointi nne juu
ya Azam yenye mechi moja mkononi na ambayo itaikaribisha Mbeya City
kwenye Uwanja wa Azam Complex Jumatano pia.
Katika mechi za ligi kuu ya Bara jana, mchezo kati ya Kagera Sugar
na Simba uliahirishwa kutokana na maji ya mvua kujaa kwenye Uwanja wa
Kambarage, wakati Ndanda na City zilitoka sare ya 1-1, Ruvu Shooting
ikaifunga JKT Ruvu 1-0 kwenye Uwanja wa Mabatini.
Goli hilo lilifungwa na Yahaya Tumbo katika dakika ya 54 kutokana
na krosi ya Michael Aidan. Ni goli la tano kwa mchezaji huyo tangu
asajiliwe Desemba mwaka jana.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani, wenyeji Coastal walilizwa 1-0 na Prisons mfungaji akiwa Jeremia Juma katika dakika ya 45.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment