Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 15 April 2015

AJALI YA BASI YAUWA MMOJA, 28 WAJERUHIWA VIBAYA


Na Hastin Liumba, NzegaJINAMIZI la ajali nchini limeendelea ambapo safari hii Basi la Kampuni ya Air Jordan lenye namba za usajiri T 650 AQZ  likitokea Mwanza kuelekea Arusha limepata ajali katika kijiji cha Ngonho kata ya Kitangili wilayani Nzega Mkoani Tabora na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 28.


Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa  kamati  ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Nzega Jackline  Liana amesema mtu aliyefariki dunia amejulikana kwa jina moja la Emmanuel ambaye alikuwa ni fundi wa Gari hilo.

Alisema sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka  hata hivyo  Dereva huyo  alitokomea kusiko julikana  baada ya kutokea ajali hiyo.

Kwa upande wake Mganga mkuu mfawidhi wa Hosiptal ya wilaya ya Nzega Erick Mbuguye alisema kuwa alipokea majeruhi 28 ambapo kati ya majeruhi wanne hali zao ni mbaya huku mmoja akiwa amekatwa mkono kulingana na jeraha alilokuwa nalo.

Alisema kuwa hali za majeruhi wengine zinaendelea vizuri huku jitihada mbalimbali za kutoa huduma zikiendelea na kuongeza kuwa kwa wale watakao kuwa na hitaji kupelekwa katika hospitali ya rufaa watapelekwa kama itahitajika kufanyika zoezi  hilo.

‘’Nimepokea majeruhi 28 na mwili mmoja lakni tunaendelea kutoa huduma na kama ikihitajika kupeleka hospital ya rufaa tutafanya lakini mpaka sasa bado na sidhani kama tutapeleka hospital ya rufaa tunaendelea kutoa huduma’’ alisema Mbuguye.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya majeruhi  wamelaani vikali baadhi ya waokoaji kuwapola mali zao badala yakutoa huduma  ya uokoaji na kuongeza kuwa serikali inapaswa kutoa elimu kubwa  kwa wananchi waishio pembezoni mwa barabara.

Frank Neto majeruhi akitokea jijini Mwanza kuelekea Arusha alisema kuwa baadi ya wananchi waishio pembezoni mwa barabara wamekuwa hawana uaminifu na utu kutokana na kufanya vitendo vya kupora watu mizigo yao badala ya kutoa huduma ya uokoaji katika eneo la tukio.

Akizungumzia sababu ya ajari hiyo Frank alisema sababu ni mwendo kasi wa Dereva ambaye aliyapita basi kadhaa huku akiwa katika eneo la kona ndipo gari hilo lilipo mshinda kulimuda na kujikuta likipinduka mara mbili.

‘’Tuseme ukweli Dereva alikuwa mwendo kasi sana alikuwa akiyapita mabasi kadhaa katika eneo hilo lenye kona ndipo gari likamshinda nilishitukia gari linakwenda kama mwendo wa nyoka,watu walipiga kelele mwenye kuomba aliomba,mwenye kulia nikashitukia gari limelia puuu’’ alisema Frenk akiwa  amelala huku majeraha mengi kichwani.

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda walisema kuwa  sababu ya ajari hiyo ni kutozingatia sheria barabarani ambapo gari hilo lilikuwa mwendo kasi huku likiwa katika eneo baya lenye kona za muundo wa ‘’S’’.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi mpaka juzi watu 866 wamepoteza maisha  na wengine  2,363 kujeruhiwa   kuanzia mwezi Januari  mwaka huu hadi Machi mwaka huu ambapo ajali zilizo tokea ni 2,116 katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Sababu ya ajari hizo zinaelezwa ni mwendo kasi kwa baadhi ya madereva na kutozingatia sheria za barabarani ikiwa na kufutika kwa baadhi ya Alama Barabarani na kuongeza kuwa sababu nyingine ni baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhimiza mwendo kasi na baadhi ya abiria kushabikia mwendo kasi.

kamanda wa jeshi la polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo bado utambuzi wa majeruhi unaendelea taarifa kamini zitatolewa.

No comments:

Post a Comment