Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 3 September 2015

NITAPAMBANA NA KERO ZENU - MGOMBEA UDIWANI


Na Hastin Liumba, Tabora
MGOMBEA Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora Kata ya Mtendeni,Yahaya Bakar amesema iwapo watamchagua katika kata hiyo atahakikisha  matatizo yanayowakabili wananchi wa kata hiyo anayashughulikia kwa kasi.

Bakari kwenye mkutano Mkuu wa Uzinduzi wa kampeni uliohudhuriwa na viongozi wa chama kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi uchaguzi ujao katika Kata ya Mtendeni.
Alisema kuwa iwapo kama watampa ridhaa atahakikisha matatizo yaliyopo katika kata hiyo kuyashughulikia kwa haraka iwezekanavyo.
Aidha kero ya maji,barabara,elimu na afya matatizo yaliyopo katika kata hiyo hivyo atahakikisha anashirikiana na wananchi, halmashauri na selikali kuyatatua.
Alisema kuwa yeye ni kazi halali katika kata hiyo anazifahamu changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi wa kata hiyo.
Hata hivyo Yahaya alibainisha kuwa tatizo la maji ni kubwa kwani, akinamama wanapata shida sana kutafuta maji na kusinda kisimani mpaka jioni.
Akizungumzia migogoro ya ardhi katika kata hiyo, alisema iwapo kama watampa ridhaa na kumpitisha kupata udiwani atahakikisha anasimamia kila mwanchi anapata haki zake kwwenye viwanja.
Yahaya alisema kwa upande wa vijana waliopo katika kata hiyo wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo watakapo mpitisha na kumpa kura nyingi ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya Tabora Mjini Lucas Masanja aliwaasa vijana kuondokana na makundi mara moja na washirikane kwa pamoja kuwachagua viongozi katika ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani.

No comments:

Post a Comment