Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 September 2015

MGOMBE AAHIDI KUJENGA KITUO CHA RADIO NA TV



Na Hastin Liumba, Uyui

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Tabora Kaskazini wilaya ya Uyui Mkoani Tabora kupitia Chama Cha  Mapinduzi Almas Maige amezindua kampeni za jimbo hilo na kuahidi kuanzisha kituo cha Radio na Televisheni ili kusadia wananchi wa jimbo hilo kupata mawasiliano ya taarifa.

Maige alitoa ahadi hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliokusanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui Isikizya ambapo alisema ili kuweka jimbo katika hadhi yake ni mhimu kupata kituo cha kurushia matangazo ili wananchi waweze kujua nini kinatokea ulimwenguni kote.

Alisema licha ya jimbo hilo kuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa huduma ya afya, miundombinu mibovu ya barabara na uhaba wa maji safi na salama, endapo atapatiwa ridhaa ya kuwa mbunge wao ataanza kushughulikia uboreshaji wa vituo vya afya.

Alisema katika vipaumbele vyake atahakikisha anamaliza tatizo la maji ambalo limekuwa kero kwa wananchi wa jimbo hilo ambao hulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita tano kutafuta huduma hiyo muhimu.

“Natambua jimbo hili lipo nyuma kimaendeleo na asilimia 85 ya wakazi wake ni wakulima wa zao la tumbaku hivyo nikiingia madarakani nitatafuta wataalamu wa kilimo ili waje kufanya utafiti wa mazao mengine ya biashara yanayoweza kustawi wilayani hapa”, alisema Maige.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Uyui Mkoani hapa Mussa Ntimizi ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Igalula wilayani humo alisema pamoja na kero hizo za  wananchi suala la ardhi limekuwa kubwa kutokana na ongezeko kubwa kwa wakazi hao ambao wengi wao ni wafugajina wakulima.

Alisema ardhi ya zamani ni tofauti na ya sasa kwa kuwa imezidi kupoteza ubora wake na watu wanaongezeka kwa kasi kubwa na hivyo uhitaji wake kuwa mkubwa kupita kawaida, ni bora serikali ya awamu ya tano itapoingia madarakani ikatafuta njia mbadala ya kushughulikia matatizo ya wakulima na wafugaji.

Ntimizi aliongeza endapo wananchi watakiamini chama hicho kiendelee kuwaongoza matatizo madogo madogo yataisha kwa kuwa nchi itakuwa katika mikono salama.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili akiwemo Haruna Kasoro alisema jimbo hilo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na miundombinu mibovu ya barabara hali inayorudisha nyuma maendeleo ya wananchi katika wilaya hiyo.

Alisema kwa sasa wanahitaji kiongozi mzalendo anayeweza kutambua shida za wananchi na kushirikana nao kuzitatua sanjari na kuboresha huduma mbalimbali na kutetea haki zao za msingi ambazo wamekuwa wakizipoteza pasipokupata msaada wowote wa viongozi wao.

No comments:

Post a Comment