Mwenge wa Uhuru
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Jengo la PSPF Golden
Jubilee Tower
Ghorofa ya Nane,
S. L. P. 8031,
7 Mtaa wa Ohio,
11481 DAR ES
SALAAM.
15/9/2015
|
Jengo la PSPF Golden
Jubilee Tower
Ghorofa ya Nane,
S. L. P. 8031,
7 Mtaa wa Ohio,
11481 DAR ES
SALAAM.
15/9/2015
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti
la Mwananchi la Tarehe 14/9/2015 toleo namba 5529 ukurasa wa 25 liliandika
habari kuhusu Mwenge wa Uhuru chini ya kichwa cha Habari “Anayeumba Mwenge wa
Uhuru” huyu hapa.
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM) ambayo ndiyo yenye dhamana ya
Mwenge wa Uhuru inapenda kuufahamisha umma kwamba habari hiyo sio ya kweli na
ni ya upotoshaji.
Mwenge
wa Uhuru ni Chombo maalum na moja ya alama nyeti za Taifa la Tanzania. Mwenge
wa Uhuru ni chombo chenye hadhi ya pekee na hivyo dhamana ya kukitengeneza haiwezi
kupewa mtu binafsi kama alivyodai Ndugu Shaban Mwinchumu na kuandikwa kwenye
gazeti la Mwananchi. Kwa sababu hiyo, kitendo cha kutengeneza au kuigiza chombo
chenye dhana na falsafa ya Mwenge wa Uhuru ni ukiukwaji wa sheria za nchi.
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ingependa kuufahamisha umma kuwa Mbio
za Mwenge wa Uhuru zilianzishwa rasmi mwaka 1964 na sio mwaka 1961 kama ilivyoandikwa katika
toleo lililotajwa. Ieleweke kwamba, Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu kuanzishwa
kwake zimekuwa zikitumika katika kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kuendelea
kujenga upendo, umoja na mshikamano wa Kitaifa bila ya kubaguana kwa misingi ya
kidini,rangi, jinsia, ukabila na itikadi za kisiasa.
Vilevile,
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuhamasisha na kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi kiuchumi
na kijamii kupitia kwenye ujumbe maalum unaotolewa kila mwaka na miradi ya
maendeleo inayobuniwa .
Wizara
pia, inapenda kuufahamisha umma wa
Watanzania kuwa michango ya fedha inayotolewa na wananchi kwa ajili ya Mbio za
Mwenge wa Uhuru si kwa ajili ya kugharamia mafuta ya Mwenge wa Uhuru
unaokimbizwa kama ilivyodaiwa na gazeti la Mwananchi. Fedha zinazochangwa ni
kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo hubuniwa na
wananchi wenyewe. Aidha, michango hiyo
hutolewa kwa hiari kutoka kwa mwananchi
mmojammoja, Vikundi, Taasisi za Umma na Binafsi, Wadau wa Maendeleo, Serikali
Kuu na Halmashauri za Wilaya.
Kwa
Taarifa hii Wizara inasisitiza kuwa madai ya Ndugu Shaban Mwinchumu ni ya
upotoshaji na hayana uhusiano wowote na masuala ya Mwenge wa Uhuru. Pia, Ndugu
Shaban Mwinchumu hajawahi kupewa kazi ya kutengeneza Mwenge wa Uhuru anayodai
kuifanya kwa muda mrefu kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Manendeleo ya Vijana
kwani hakuna Wizara hiyo kwenye orodha ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mwisho
kabisa Wizara inawataka waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya
habari kuandika habari kwa usahihi zenye kujenga Umoja wa Kitaifa kwa kupata
ufafanuzi wa kila upande ili habari itoe picha halisi badala ya kuegemea upande
mmoja kwani kwa kuegemea upande mmoja hupotosha jamii na si maadili ya taaluma
ya habari.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
RECO Engineering nao wakasema haya:
No comments:
Post a Comment