Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 9 September 2015

IDADI YA WAKIMBIZI YAONGEZEKA KAMBI YA NYARUGUSU


Kigoma. Idadi ya wakimbizi kutoka Burundi wanaokimbia nchi yao na kuingia nchini Tanzania imefikia 91,661 hadi kufikia jana Jumanne.  Wakimbizi hao kwa sasa wamehifadhiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa vyombo vya habari inasema kuwa tangu wakimbizi hao waanze kuingia nchini mwezi Aprili mwaka huu, wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine wameendelea kupokea wakimbizi na kwamba wanawapa hifadhi na huduma nyingine muhimu.

“Hali ya ulinzi na usalama katika Kambi ya Nyarugusu na maeneo yanayoizunguka imeimarika ambapo upo usalama wa kutosha,” inasema taarifa hiyo na kuongeza:

“Kazi hii inafanywa na polisi kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi vinavyojumuisha baadhi ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hii.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Msemaji wa Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga, serikali kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) imeimarisha huduma hizo kwa kuongeza idadi ya watendaji, vifaa na dawa.

Pia inasema huduma za afya zimeimarishwa ambapo hali hiyo imesaidia kudhibiti magonjwa ya mlipuko na kukabiliana na magonjwa mengine yasiyo ya mlipuko.

“Kabla ya kufikia idadi hii ya sasa, wengi wa wakimbizi walianza kuingia kwa maelfu kupitia kijiji cha Kagunga kilichopo mpakani na nchi ya Burundi ambapo idadi ilianza kupungua  kidogo lakini kwa siku za hivi karibuni wakimbizi wameendelea kuingia wakiwa katika vikundi vidogovidogo,” inasema taarifa hiyo.

CREDIT: MWANANCHI


No comments:

Post a Comment