Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 21 June 2015

MAPIGANO MAKALI YAENDELEA MOGADISHU


Mapigano makubwa yameripotiwa kwenye mji kuu wa Somalia Mogadishu baada ya shambulizi la gari la kujitoa mhanga kutokea karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo.

Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab waliingia jengo lililo karibu na makao hayo makuu ya ujasusi, na kukana madai ya al-Shabab kuwa waliingia makao ya ujasusi yenyewe.
Hakuna ripoti zozote zilizotolewa za watu kuuawa au kujeruhiwa
Al-Shabab wameapa kuongeza mashambulzii dhidi ya serikali ya Somalia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan ambao ulianza siku ya Jumatano.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment