Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 1 June 2015

KIM KARDASHIAN NI MJAMZITO

Kim Kardashian
Nyota wa kipindi cha runinga nchini Marekani, Kim Kardashian, ambaye ameolewa na msanii Kanye West amefichua siri katika kipindi cha Keeping up with the Kardashians.

Kim Kardashian amefichua kwamba amefanya ukaguzi wa damu na kubaini kwamba ni mjamzito.
''Nilifanya ukaguzi wa damu na nimegundua kwamba mimi ni mjamzito'',alimwambia dadaake Khloe Kardashian.
Kanda hiyo ya Video pia ilionyesha akienda kufanyiwa ukaguzi.
Huyu atakuwa mwamna wa pili wa nyota hao ambao walipata mtoto wao wa kwanza North West mwezi Juni mwaka 2013.
Kanye West na Kim Kardashian
Hakuna maelezo kuhusu ni lini mwana huyo atazaliwa.
Kabla ya kanda hiyo ya video kuonyeshwa ,Kim alituma ujumbe wake wa Twitter akisema kwamba ana habari njema za kutangaza.
Katika kipindi hicho Kim amekuwa akisema kwamba imekuwa vigumu kwa yeye na Kanye kupata mtoto mwengine.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment