Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 4 June 2015

JACK WARNER AAPA KUFICHUA UFISADI FIFA

Jack Warner amesema atafichua kila anachojua kuhusu ufisadi ndani ya FIFA
Aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner amesema katika hotuba ya kushangaza aliyotoa katika runinga kwamba atafichua kila anachojua kuhusu ufisadi katika shirikisho hilo.

Bwana Warner ambaye alisema kuwa anahofia maisha yake pia amesema kuwa anaweza kuwahusisha maafisa wa FIFA na uchaguzi mkuu katika taifa la Trinidad and Tobbago mwaka 2010.
Maafisa wa FIFA wanaotuhumiwa na ufisadi
Ni mmoja wa watu 14 walioshtakiwa na Marekani kuhusiana na ufisadi katika FIFA.
Mmoja wa maafisa wakuu wa FIFA na shahidi muhimu Chuck Blazer alikubali kuchukua hongo.
Chuck Balzer akiwa na Sepp Blatter
Afisa huyo alikiri kufanya hivyo mnamo mwaka 2013,ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa ambayo yameikabili FIFA na kumlazimu rais wake Sepp Blatter Kujiuzulu.
Idara ya mahakama ya Marekani inadai kuwa watu 14 walioshtakiwa walikubali hongo ya zaidi ya dola milioni 150 katika kipindi cha miaka 24.
Chuck Blazer amekiri kupokea hongo
Watu wengine wanne walikuwa tayari wameshtakiwa akiwemo Blazer.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment