Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 17 August 2015

UKAWA WAZOA WANACHAMA WAPYA 203


Na Hastin Liumba, Kaliua

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umeendelea kuzoa wanaCCM ambapo zaidi ya wanachama wa CCM  203 wa kata ya Kanoge jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua kurudisha kadi za CCM na kujiunga CHADEMA.

Tukio hilo limetokea kijiji cha Kanoge kata ya Kanoge wilayani Kaliua katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhutubiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa Francis Msuka.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Peter Mwakibete alitangaza rasmi kujitoa CCM na kuhamia CHADEMA akiwa na wanachama lukuki aliokuwa nao ndani ya CCM.
Akielezea sababu za kujitoa Mwakibete alisema yeye alikuwa mtetezi namba moja wa haki za wananchi katika kata hiyo lakini jitihada zake mara nyingi zilikuwa zinakwamishwa na viongozi wenzake jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika utendaji wake.
Alieleza kuwa zipo kero nyingi zinazokwamisha maendeleo ya kata ikiwemo kukithiri kwa vitendo vya uonevu vinavyofanywa na viongozi wenzake sambamba na michango ya mara kwa mara isiyofuata utaratibu.
 'Nimeamua kujiunga na timu ya watu wenye dhamira ya kweli ya kutetea maslahi ya wananchi, uonevu umezidi, hakuna mwana CCM anayekemea, naamini chama pekee kisichopenda vitendo hivyo ni CHADEMA, ndio maana nimeamua kujiunga nacho', alisema
Wengine waliojitoa ndani ya chama hicho na kutimkia CHADEMA ni uongozi mzima wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV CCM) wakiongozwa na Mwenyekiti  wa UVCCM kata ya Kanoge Msesa Damas, Katibu wake Lucas Mbeyu na wajumbe wote wa jumuiya hiyo wakiwemo Maria Lucas na Nigalule Kayumbu.
Akihutubia mkutano huo Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Tabora Francis Msuka alisema wakati wa mabadiliko ukifika hakuna anayeweza kuzuia ndio maana wananchi wengi sasa wanakimbilia UKAWA kwa sababu huu ni wakati wa mabadiliko.
Kada na Mhamasishaji wa chama hicho mkoani hapa Daud Elisha aliwataka wananchi kuwapuuza wote wanaobeza ujio wa wanachama wapya ndani ya UKAWA akiwemo mgombea urais wa CHADEMA Edward Lowassa kwani wote wanaojiunga humo ni wapenda maendeleo na wanataka mabadiliko ya kweli.
Naye  diwani wa kata ya Ipole wilayani Sikonge anayemaliza muda wake Hijja Mohamed ambaye pia ni miongoni mwa wagombea ubunge wa jimbo la Sikonge alisema huu si wakati wa kufumbia macho viongozi wasiowajibika.

No comments:

Post a Comment