Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 31 August 2015

GESI NYINGI YAGUNDULIWA MISRI

shughuli za kuchimba gesi  mwambao wa Misri
Kampuni ya mafuta ya Italia, Eni, inasema imegundua katika mwambao wa Misri, moja kati ya visima vikubwa kabisa duniani vya gesi.
Kampuni hiyo imesema kisima hicho kiitwacho Zohr, kiko mita 1,500 chini ya bahari, na inakisiwa kuwa kina mita za mjazo bilioni 850 za gesi.
Mkurugenzi mkuu wa Eni amesema kisima hicho kipya kinaweza kuwa mmoja kati ya ugunduzi mkubwa kabisa wa gesi duniani na kitasaidia kukidhi mahitaji ya gesi ya Misri kwa miongo kadha ijayo.
Kampuni ya Eni ya Utaliana, ambayo ina haki kamili ya kuchimba kisima hicho, ni kampuni kubwa kabisa ya kigeni Afrika katika sekta ya mafuta na gesi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment