Hisa nchini Uchina zimeendelea kushuka huku wasiwasi kuhusu ukuwaji mdogo wa uchumi nchini humo pamoja na msukosuko wa soko hilo ukisababisha hofu miongoni mwa wafanyibiashara.
Soko la hisa nchini humo lilifunga chini ya asilimia nane na nusu na kuongeza hasara iliopatikana wiki iliopita.
Masoko nchini Uchina yamenguka kwa zaidi ya thuluthi moja tangu mwezi Juni.
Barani Asia ,masoko ya hisa pia yalianguka kabla ya kufungwa kwa biashara siku ya jumatatu huku masoko ya barani Ulaya yakifunguliwa huku hisa zikiwa chini.
Vyombo vya habari barani Asia yametaja kuanguka kwa soko siku ya jumatatu kama siku nyeusi.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment