Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 17 August 2015
MGOMBEA CHADEMA AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO TABORA
Na Hastin Liumba,Tabora
KADA wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Martin Musa amesema endapo atashinda nafasi ya udiwani kata ya Mwinyi ataanzisha kituo cha vijana cha mchezo wa mpira wa miguu na mingineyo.
Musa alisema hayo wakati akifanya mahojiano na gazeti hili ofisi za CHADEMA kanda ya magharaibi mkoani hapa.
Alisema yeye ni mtu wa michezo hivyo asingependa kata yake haishiriki mchezo hata mmoja ikiwemo soka.
Musa alisema hadi sasa kata hiyo haina mashindano yoyote hasa soka hivyo vijana wengi wamekuwa wakikaa vijiweni tu.
Alisema atatumia fursa zilizopo kuhakikisha anaanzissha kituo cha michezo ili kuunganisha vijana kwenye michezo mbalimbali.
Alisema kituo hicho licha soka kupewa kipaumbele bado atashirikisha na michezo mingine kwani dhamira anayo.
Hata hivyo atahakikisha anaanzisha na kufufua viwanja ambavyo vingine vimekuwa huku maeneo mengine yakiwa hayana kabisa viwanja vya michezo.
Alisema ataomba uongozi wa halmashauri ya manispaa kupima viwanja ili vijana waweze kupatiwa maeneo ya michezo.
Musa alisema licha ya kuwa atakuwa na kazi ya kutekeleza ilani ya chama kwenye sekta nyingine bado michezo ni sehemu ya ilani ya chama chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment