Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 17 August 2015
MRITHI WA SAID NKUMBA ASEMA ANASUBIRI ILANI
Na Hastin Liumba, Sikonge
KADA wa chama mapinduzi (CCM) aliyepata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM uchaguzi mkuu oktoba 25 mwaka huu katika jimbo la Sikonge mkoani Tabora, George Joseph Kakunda amesema anasubiri kukabidhiwa ilani ya chama chake ndipo atataja vipaumbele vyake.
Kakunda alisema hayo wakati akiongea na wanCCM na wananchi waliofika kumlaki wilayani Sikonge kwamba kwa sasa hawezi kusema chochote hadi hapo atakapokabidhiwa na chama chake ilani ya uchaguzi.
Mgombea huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi wa Wizara ya Maji Makao Makuu jijini Dar es salaam aliwasili wilayani humo majira ya asubuhi ambapo alipokelewa katika kijiji cha Pangale na msafara wake kuanza kuelekea mjini Sikonge ukipitia katika kata za Mpombwe, Tutuo, Mole, Usanganya na Sikonge.
Kakunda alisema ana dhamira ya dhati kuwatumikia wana Sikonge na yupo tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu katika nafasi hiyo ya ubunge.
‘Ndugu zangu wana Sikonge nipo tayari kuwatumikia, nipo tayari kushirikiana nanyi kupeperusha bendera ya CCM kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hili, naamini tukishikamana kwa pamoja tutafanikiwa katika kujiletea maendeleo.’, alisema.
Alieleza amejipanga vizuri kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama chake kwa kuhakikisha anayapa kipaumbele yale yote yaliyoainishwa ndani ya ilani hiyo ili kuwaletea maendeleo wananchi pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile.
‘Mimi sina mkakati wowote binafsi, ila nikifanikiwa kushinda hapo mwezi Oktoba 25 mwaka huu nitatekeleza yale yote yaliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya chama changu kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya wilaya hii’, aliongeza.
Katibu wa CCM wilayani Sikonge Selemani Majilanga alibainisha wazi kuwa Kakunda ni mrithi sahihi wa mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake Said Nkumba.
Alisema leo hatutakuwa na mengi kwani mkiutano wetu ulikuwa wa mapokezi tu nadhani tusubirie wakati wa kampeni ndipo tutakuwa mengi ya kutamka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment