Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 13 August 2015
UKAWA MANISPAA TABORA WAKUTANA
Na Hastin Liumba, TaboraVYAMA vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) jimbo la Tabora mjini, wamekutana na kujadili kwa kina jinsi ya kuachiana jimbo na viti vya udiwani.
Jimbo hilo la Tabora mjini lina jumla ya kata 29 umoja huo unaundwa na vyama vya NLD,NSSR-Mageuzi,CHADEMA na CUF.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za NSSR-Mageuzi chama cha NLD wameomba kuachiwa kata moja ya Chemchem huku NSSR-Mageuzi wameomba kuachiwa kata moja ya Kitete .
Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Tabora mjini Mustafa Mhozya na katibu wa NSSR-Mageuzi Said Lengwe walikiambia kikao hicho kuwa wamejitathimini na kuona wanatosha katika kata hizo.
Vyama vya CHADEMA na CUF nao walikubaliana katika kata 27 zilizobaki likiwemo jimbo la Tabora mjini wakutane leo kuangalia katika kata hizo wanaachiana wapi ikiwemo jimbo.
Katika nafasi za jimbo waliopita katika kura za maoni kupitia CHADEMA ni Peter Mkufya wakati kwa upande wa CUF aliyepita kura maoni ni David Mtinya.
Wakijadili kwa kina viongozi hao walikubaliana kuwa kitu kimoja ili CCM ifikie mahali iondoke madarakani katika jimbo la Tabora mjini wanapaswa kuweka mbele maslahi ya wananchi na kamwe kusiwe na ubanafsi kwenye maamuzi hayo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wilaya wa CHADEMA Saimon Lameck alikiambia kikao hicho kuwa wafikie makubaliano ambayo yatasaidia kupata ushindi wa kishindo.
Lameck alisema endapo watafanya maamuzi yasiyo na tija basi watambue CCM itashinda kata zote likiwemo jimbo hivyo wafanye maamuzi sahihi na kuweka mtu anayekubalika kwa wananchi ili ukawa tushike halmashauri manispaa.
Alisema UKAWA taifa wameleta vigezo ambavyo vitatumika katika mgawanyo wetu ambao ni kuwfanya maamuzi ya kuweza kupata kura nyingi za urais, uteuzi uangalie ushindi chaguzi za serikali za mitaa,sifa za mgombea na nguvu ya mgombea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment