Paulo Wanchope
Meneja wa timu ya taifa ya mpira wa miguu wa Costa Rica, Paulo Wanchope, amebwaga manyanga siku moja baada ya kuhusika na tukio la kupigana wakati wa mchezo huko Panama.
Paulo anaonekana katika mkanda wa video akiwa na hasira huku akifungua geti karibu na uwanja ambapo alianza kupambana na bwana mmoja kabla ya wanausalama kuingilia kati.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa meneja huyo hakua na furaha na muamuzi wa mchezo huo,pamoja na hayo mchezo huo uliisha kwa matokeo ya bila kufungana.
CREDIT: BBC

No comments:
Post a Comment