Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 13 August 2015

SAID NKUMBA AJIUNGA CHADEMA

Said Nkumba (katikati) akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na afisa wa chama hicho kanda ya magharibi Daud Ndelwa mara baada ya kujiunga na chama hicho,kushoto kwake ni Lazaro Mayani ambaye ni mwenyekiti BAVICHA Mkoa.

Na Hastin Liumba, TaboraMBUNGE wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora (CCM) Said Nkumba amehama chama hicho na kujiunga na CHADEMALEO.
Nkumba alijunga na CHADEMA kufuati kutoridhishwa na mwenendo wa CCM ambapo akikabidhiwa kadi namba 24669001.

Akiongea kwa ufupi Nkumba alisema amefadhaishwa na kusikitishwa jinsi CCM inavyoendeshwa na kwamba kama hua fedha basi uongozi hupati.

Alisema katika kura za maoni alijionea mwenyewe jinsi wanaCCM ambao walikuwa wanamwambia wanataka fedha ndipo wamchague.

Aidha kitendo cha yeye kusimama kidete kusemea na kutetea wakulima wa tumba nachpo ndicho chanzo cha yeye kuchukukiwa.

Nkumba alisema ilifikia mahali viongozi wa CCM mkoa wa Tabora walikuwa wanakuja Sikonge kuhakikisha yeyeanaanguka.

Alisema viongzo hao walikuwa wanatoa fedha na pikipiki ili yeyetuanaondoka katika nafasi ya ubunge na kuanguka kwenye kura ya maoni.

Nkumba pia alitamka kujiuzulu nafasi zake za makamu mwenyekiti wa bodi ya tumbaku nchini,mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM,mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Tabora.

Nyingine ni kiongozi wa Tanzania kwanza ndani ya bunge na kwamba kuanzia sasa yeye ni mwanachama mpya wa CHADEMA.

Alisema amejiunga na CHADEMA siyo kwenda kutafuta vyeo bali kama mwanachama wa kawaidd na kama atahitajika na viongozi kwa nafasi hata ya katibu kata anafanya kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment