Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 July 2014

MAREKANI YAIWEKEZA VIKWAZO ZAIDI URUSI

Rais Obama ajaribu kuiadhibu Urusi akisema Moscow yaihujumu Ukraine, Je Atafanikiwa?
Marekani imetangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi ikilenga secta zake za Ulinzi, fedha na makampuni ya kawi.
Baadhi ya waliolengwa na vikwazo hivyo vikali ni kampuni kubwa ya mafuta , Rosneft,makampuni ya ulinzi na hata maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Urusi.
Amesema Urusi ilitarajiwa ikomeshe upenyezwaji wa silaha na wapiganaji kutoka Urusi wenye lengo la kuendeleza mapigano huko mashariki mwa Ukraine.Rais Obama amesema ni kwa sababu utawala wa Moscow badala ya kuchukua hatua za kusaidia kumaliza mgogoro wa mashariki mwa Ukraine inaelekea inaendelea kuuchochea.
Rais Putin asema vikwazo vya Marekani kwa Urusi ni mwiba utakaoichoma pia Marekani
Rais wa Urussi , Vladimir Putin, ambae kwa sasa yuko Brazil kwa mkutano wa kiuchumi wa mataifa ya Brics -- amejibu kwa kusema vikwazo hivyo vitaaathiri pia maslahi ya Marekani na kuzorotesha zaidi uhusianoo baina ya mataifa hayo.
Kwa upande wao Viongozi wa nchi za umoja wa Ulaya nao wamesema wataongeza vikwazo dhidi ya Urussi kwani inaendelea kuuhujumu utaifa wa Ukraine.

Ulaya na Marekani ni baadhi ya nchi zinazotegemea zaidi kawi ya gesi kutoka Urusi.(BBCSWAHILI)

No comments:

Post a Comment