Hata kama baba zao ni maarufu kama wao au ni watu wa kawaida tu wanaopenda kuwaunga mkono watoto wao katika matukio makubwa, inapendeza sana kuona watu maarufu katika filamu na muziki wakiwa na baba zao mahali popote.
Hebu watazame hawa...
Stella McCartney
Stella alikuwa na baba yake ambaye ni supastaa wakati alipokuwa katika maonyesho ya picha za maisha - A Life in Photographs: An Exhibition of Photography yaliyoandaliwa na Linda McCartney mwezi Juni 2011.
Zoë Kravitz
Mwigizaji huyu alishereheka akiwa na baba yake, Lenny, ambaye ni mwanamuziki wa rock, baada ya Tuzo za Filamu za MTV Juni 2010.
Alexander Skarsgard
Staa huyu wa mmuvi ya Avengers aliongozana na baba yake ambaye ni mwigizaji pia, Stellan, katika maonyesho ya filamu ya Los Angeles Aprili 2012.
Taylor Swift
Baba yake Taylor, Scott, akiwa amepozi naye katika tukio la CMT mjini Nashville mnamo Oktoba 2008.
Angelina Jolie
Angelina akiwa amekumbatiwa na baba yake, mwigizaji Jon Voight, katika maonyesho ya Vanity Fair mwezi Februari 2001.
Jordin Sparks
Baba yake Jordin, mchezaji wa zamani wa NFL Phillippi Sparks, ndiye aliyetoka naye wakati wa uzinduzi wa filamu ya Sparkle huko Los Angeles mwezi Agosti 2012.
Lady Gaga
Lady Gaga alikuwa na baba yake, Joe Germanotta, pembeni yake kwenye zulia jekundu wakati wa tuzo za MTV VMA Agosti 2013.
Kate Winslet
Baada ya kutwaa tuzo ya Oscar mwezi Februari 2009, Kate Winslet alisherehekea na baba yake, Roger, pale Vanity Fair .
Jake Gyllenhaal
Jake alihudhuria tukio la Rock the Vote akiwa na baba yake ambaye ni muongoza filamu, Stephen, jijini Los Angeles mwezi Septemba 2004.
Jennifer Aniston
Jennifer alipambwa na tabasamu wakati akiwa na baba yake, John Aniston, wakati alipotunukiwa nyota katika Hollywood Walk of Fame mwezi Februari 2012.
Blake Lively
Blake alikwenda na baba yake, Ernie Lively, kwenye uzinduzi wa The Sisterhood of the Traveling Pants jijini Los Angeles mwezi Mei 2005.
Liv Tyler
Liv alikuwa na baba yake, mwimbaji kiongozi wa kundi la Aerosmith Steven Tyler, wakati wa uzinduzi wa filamu ya Super jijini Los Angeles mwezi Machi 2011.
Kate Hudson
Kate na baba yake Kurt Russell walikuwa pamoja jijini Los Angeles mwezi Oktoba 2007.
Sandra Bullock
Sandra akiwa na baba yake, John, katika uzinduzi wa filamu ya Forces of Nature jijini Los Angeles mwezi Machi 1999.
Miley Cyrus
Miley alipozi kwenye zulia jekundu akiwa na baba yake, Billy Ray, katika Tuzo za Muziki za Amerika - AMA mwezi Novemba 2013.
George Clooney
George Clooney na baba yake ambaye wanafanana, Nick, walishereheka pamoja baada ya uzinduzi wa filamu yake ya The Ides of March jijini New York Oktoba 2011.
Kelly Osbourne
Baba yake Kelly, mwanamuziki maarufu wa rock Ozzy Osbourne, alimsindikiza bintiye katika onyesho lake jijini Los Angeles Mei 2014.
Laura Dern
Laura alikanyaga mazulia mekundu akiwa na baba ake mwigizaji, Bruce, wakati wa msimu wa utoaji tuzo mbalimbali mwaka 2014, ikiwemo Tuzo za SAG mwezi Januari.
Nicky na Paris Hilton
Nicky na Paris Hilton walipiga picha ya pamoja na baba yao, Rick, wakati wa sherehe ya uzinduzi wa manukato ya Paris mwezi Desemba 2004.
Chelsea Clinton
Chelsea akitabasamu pembeni ya baba yake, rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton, katika usiku wa uchangishaji fedha za mfuko wa familia jijini London mwezi Mei 2012.
Prince Harry na Prince William
Wanafamilia ya Kifalme wadogo walisafiri hadi Uswisi na baba yao, Prince Charles, mwezi Machi 2005.
Ashton Kutcher
Ashton Kutcher alikwenda na baba yake, Larry, kwenye uzinduzi wa filamu yake ya Just Married mwezi Januari 2003.
Bruno Mars
Bruno Mars na baba yake, Peter Hernandez, wakiwa katika pozi wakati wa sherehe za tuzo za MTV VMA mwezi Agosti 2013.
Kate Middleton
Baba yake Kate Middleton, Michael, alimuongoza bintiye wakati wa sherehe yao ya ndoa na Prince William jijini London mwezi Aprili 2012.
Ben Stiller
Ben alikwenda kushuhudia game ya timu ya New York Knicks akiwa na baba yake, Jerry, mnamo Aprili 2012.
Shakira
Shakira akimbusu baba yake, mwimbaji William Mebarak Chadid, wakati walipoimba pamoja kwenye sherehe za utoaji wa tuzo jijini Las Vegas mwezi Novemba 2011.
Rashida Jones
Baba yake Rashida, Quincy Jones, ndiye aliyetoka naye wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Celeste & Jesse Forever jijini Los Angeles Juni 2012.
Amber Heard
Amber alikwenda na baba yake, David, kwenye sherehe za tuzo za Golden Globes mwezi Januari 2014.
Adrian Grenier
Adrian akipozi na baba yake, John Dunbar, kwenye uzinduzi wa documentary yao ya Shot in the Dark mwezi Mei 2007.
Lupita Nyong'o
Lupita aliamua kwenda kupotea tuzo yake akiwa na baba yake, Peter Nyong'o Sr., wakati alipokabidhiwa Tuzo ya Oscar huko Governors Ball mwezi Machi 2014.
Allison Williams
Allison akifurahia kampani ya baba yake, mtangazaji wa kituo cha televisheni cha NBC Brian Williams, katika sherehe ya Girls mwezi Januari 2014.
Matt Damon
Matt akifurahia jambo na baba yake, Kent, wakati wa upigaji picha wa filamu yake ya The Bourne Supremacy kwenye sherehe za Deauville Film Festival mwezi Septemba 2004.
Chris Pine
Chris na baba yake, Robert, wakiwa kwenye uzinduzi wa filamu ya Star Trek Into Darkness jijini Los Angeles Mei 2013.
Poppy Delevingne
Poppy akipigwa busu na baba yake, Charles, katika sherehe mojawapo ya mitindo jijini London Aprili 2014.
Jessica na Ashlee Simpson
Wanadada hao wakitabasamu pamoja na baba yao, Joe, jijini New York mwezi Machi 2005.
Natalie Portman
Natalie alipata kampani nzito ya baba yake, Avner Hershlag, wakati wa Tuzo za Critics' Choice Movie mwezi Januari 2011.
Lena Dunham
Wakati wa Tuzo za Directors Guild of America mwezi Februari 2013, Lena
Dunham aliongozana na baba yake, Carroll, ambaye ni mpaka rangi mashuhuri.
Nicole Richie
Nicole na baba yake ambaye ni mwanamuziki maarufu duniani, Lionel, waliimba pamoja huko Las Vegas mwezi Aprili 2012.
Lily Collins
Lily alikuwa na baba yake, mwanamuziki mashuhuri Phil Collins, wakati wa uzinduzi wa muvi yake ya Mirror Mirror mwezi Machi 2012.
Joseph Gordon-Levitt
Joseph na baba yake, Dennis, wakiishangilia timu ya LA Lakers mwezi Januari January 2013.
Jaden na Willow Smith
Jaden na baba yake Willow wakiwa na baba yao, Will Smith , wakati wa Tuzo za MTV VMA mwezi Agosti 2013.
Kate Moss
Baba yake Kate, Peter, alikuwa pembeni yake wakati wa maonyesho ya mavazi jijini London maarufu kama Kate Moss : The Collection mwezi Septemba 2013.
Jennifer Lopez
Jennifer akibembea begani kwa baba yake, David, wakati wa ufunguzi wa mgahawa wake wa Madre's huko Pasadena Aprili 2002.
Kaley Cuoco
Kaley alikwenda na baba yake, Gary, kwenye uzinduzi wa The Big Bang Theory huko Los Angeles mwezi Februari 2010.
Katy Perry
Katy na baba yake, Keith Hudson, walitembea kwenye zulia jekundu pamoja wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya muziki jijini Hollywood mwezi Juni 2012.
Anna Faris
Anna akitabasamu na baba yake, Jack, katika tukio la Rolling Stone mjini Indianapolis mwezi Februari 2012.
Scott Eastwood
Scott alikuwa na baba yake, Clint, katika uzinduzi wa filamu ya Flags of Our Fathers jijini Los Angeles Oktoba 2006.
Julia Louis-Dreyfus
Julia alikwenda na baba yake, William, katika upigaji picha za muvi jijini New York Mei 2014.
Mark Ruffalo
Mark alikuwa reale kwa ya pili na baba yake, Frank, katika sherehe za Foxcatcher wakati wa Maonyesho ya Filamu ya Cannes mwezi Mei 2014.
Bryce Dallas Howard
Baba wa Bryce ambaye ni supastaa, Ron, aliongozana na bintiye katika upigaji picha za muvi huko New York mwezi Oktoba 2013.
Emilio Estevez
Emilio Estevez na baba yake Martin Sheen walikuwa pamoja kwenye Tuzo za Critics' Choice Januari 2007.
Ivanka Trump
Ivanka alikuwa na baba yake, Donald, pembeni yake katika uzinduzi huko New York Aprili 2014.
Amber Tamblyn
Amber alikuwa kila mahali mwezi Novemba 2011 wakati baba yake mwigizaji Russ Tamblyn, alipotunukiwa nyota kwenye orodha ya Hollywood Walk of Fame.
Reese Witherspoon
Reese Witherspoon alikuwa na baba yake, John, wakati alipotunukiwa nyota kwenye orodha ya Hollywood Walk of Fame mwezi Desemba 2010.
Zach Braff
Baba yake Zach, Harold, aliongozana na kijana wake kwenye Tuzo za Tony mwezi Juni 2014.
Spencer Grammer
Spencer alikwenda na baba yake, Kelsey, katika uzinduzi wa tamthiliya ya Boss ambayo baba yake anashiriki huko Los Angeles Oktoba 2011.
Sofia Coppola
Sofia akipata busu kutoka kwa baba yake, Francis Ford Coppola, wakati wa Tuzo za Directors Guild mwezi Februari 2004.
Alexa Chung
Alexa na baba yake, Philip, waliongozana kwenye maonyesho ya London mwezi Mei 2012.
Lauren Conrad
Lauren alikuwa na baba yake, Jim, wakati akijiandaa na mchezo wa timu yake ya LA Dodgers mwezi Juni 2009.
No comments:
Post a Comment