Miley Cyrus akiwa katika pozi la upendo na mama yake, Tish, katika sherehe mojawapo ya Oscars mwezi Februari 2013.
Jay Z
Jay Z 'hajaopoa' bali amekumbatia mama yake, Gloria Carter, katika tukio la hisani mwezi Septemba 2011.
Justin Timberlake
Mama yake Justin Timberlake , Lynn Harless, alimsindikiza mwanaye kwenye sherehe za tuzo za Oscars mwaka 2011.
Brad Pitt
Brad Pitt alikwenda na mama yake, Jane, kwenye zulia jekundu wakati wa Tuzo za Oscars 2012.
Jared Leto
Mama mrembo wa Jared Leto , Constance, aliongozana naye kwenye Tuzo za SAG mwezi Januari 2014.
Usher Raymond
Usher aliongozana na mamaye, Jonetta Patton, kwenye Tuzo za MTV European Music mwaka 2004.
Leonardo DiCaprio
Leonardo DiCaprio alikuwa na mama yake, Irmelin, kwenye sherehe pale Vanity Fair baada ya tuzo za Oscars mwezi Machi 2014.
Kate Hudson
kumbe Kate Hudson kautoa urembo kwa mama yake, Goldie Hawn . Cheki hapa wanavyopendeza wakati wa Chakula cha Usiku cha Waandishi wa Habari wa Ikulu mwaka 2012.
Ryan Gosling
Ryan Gosling kila wakati huongozana na mama yake, Donna, kwenye matukio mbalimbali. Wawili hao wanaonekana wakitabasamu wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Ides of March mwaka 2011.
Katie Holmes
Katie Holmes na mama yake, Kathleen, walihudhuria shoo ya Max Mara wakati wa Wiki ya Urembo ya Milan 2011.
Lupita Nyong'o
Lupita Nyong'o aliongozana na mama yake, Dorothy, wakati wa sherehe za Independent Spirit Awards mwezi Machi 2014.
Gwyneth Paltrow
Blythe Danner akimbusu binti yake Gwyneth Paltrow wakati wa tukio la hisani jijini New York mwaka 2008.
Charlize Theron
Charlize Theron akipozi na mama yake, Gerda, kwenye zulia jekundu mwaka 2009.
Beyoncé Knowles
Beyoncé Knowles na mama yake, Tina, wakitembea pamoja Septemba 2011 wakati wa uzinduzi wa bidhaa zao pale House of Deréon.
Jessica Simpson
Jessica Simpson na mama yake, Tina, katika pozi wakati wa uzinduzi wa mavazi yake mwaka 2010.
Scarlett Johansson
Scarlett Johansson alikwenda na mama, Melanie, kwenye sherehe za baada ya tuzo za Tony Awards mwaka 2004 jijini New York.
Gisele Bündchen
Gisele Bündchen akiwasili New York na mama yake, Vania Nonnenmacher, katika uzinduzi wa filamu ya Taxi mwezi Oktoba 2004.
Britney Spears
Britney Spears na mama yake, Lynne, walihudhuria uzinduzi wa filamu ya Four Feathers mwezi Septemba 2002.
David Beckham
David Beckham akiwa na mama yake, Sandra, wakati wa mechi ya La Liga nchini Hispania Januari 2007.
Sienna Miller
Sienna Miller akimbusu mama yake, Jo, Juni 2007 wakati wa Tuzo za Glamour Women of the Year jijini London.
Jennifer Lopez
Jennifer Lopez akiwa na mama yake, Guadalupe, wakati wa Tuzo za 10 za ACE Oktoba 2006.
Eva Longoria
Eva Longoria alikwenda na mama yake, Ella, wakati wa Tuzo za ALMA mwezi Septemba 2013.
Kim Kardashian
Kim Kardashian na mama yake, Kris Jenner, walihudhuria tukio la Hollywood Reporter 's Women in Entertainment mwezi Desemba 2013.
Rachel Bilson
Rachel Bilson alikuwa na mama yake, Janice, wakati wa uzinduzi wa filamu ya Last Kiss jijini Los Angeles mwezi Septemba 2006.
Hilary na Haylie Duff
Hilary Duff na Haylie Duff walihudhuria uzinduzi wa filamu ya Material Girls jijini New York wakiwa na mama yao, Susan, mwezi Agosti 2006.
Ryan Seacrest
Ryan Seacrest alitunikiwa nyota moja kwenye orodha ya Hollywood Walk of Fame mwezi Aprili 2005 huku mama yake, Connie, akishuhudia.
Tom Cruise
Tom Cruise alikwenda na mama yake, Mary, kwenye Tuzo za Golden Globe mwezi Januari 2011.
Kate Moss
Kate Moss akiwa na mama yake, Linda, kwenye tukio la Rimmel jijini London Septemba 2011.
Zoe Saldana
Zoe Saldana na mama yake, Asalia Nazario, wakifurahia Juni 2010 wakati wa Tuzo za Crystal + Lucy jijini Los Angeles.
Taylor Swift
Taylor Swift na mama yake, Andrea, walikuwa pamoja kwenye Tuzo za Grammy Januari 2010.
Channing Tatum
Channing Tatum alihudhuria uzinduzi wa filamu ya Fighting jijini New York akiwa na mama yake, Kay, mwezi Aprili 2009.
Jennifer Garner
Jennifer Garner na mama yake, Pat, walihudhiria mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Akinamama Duniani (State of
the World's Mothers Report) kwenye ukumbi wa Rosemont Center mwezi Mei 2009.
Joaquin Phoenix
Mama wa Joaquin Phoenix , Arlyn, alikuwa pembeni ya mwanawe wakati wa Tuzo za Golden Globes mwezi Januari 2014.
Jonah Hill
Jonah Hill alikuwa na kampani ya nguvu ya mama yake, Sharon, wakati wa tuzo za Oscars Machi 2014.
Miranda Kerr
Miranda Kerr akiwa na mama yake, Therese, katika tukio la David Jones Spring/Summer Collection Launch huko Sydney, Australia mwezi Agosti 2009.
Michael Fassbender
Michael Fassbender alikuwa na mama yake, Adele, pembeni yake wakati wa Tuzo za Oscars mwezi Machi 2014.
Lorde
Lorde yuko na mama yake, Sonja, katika pozi zito wakati waliponyakua tuzo mbili za Grammy mwezi Januari 2014.
Blake Lively
Blake Lively akifurahi na mama yake, Elaine, wakati wa Tuzo za 61 za Primetime Emmy Awards mwezi Septemba 2009.
Drake
Mama wa Drake, Sandi Graham, aliungana na mwanaye kwenye zulia jekundu wakati wa Tuzo za Juno jijini Toronto, Canada mwezi Machi 2011.
Anne Hathaway
Anne Hathaway na mama yake, Kate McCauly, wakikumbatiana nyuma ya jukwaa wakati wa tukio la hisani Aprili 2005 jijini New York.
Kathy Griffin
Kathy Griffin na mama yake, Maggie, katika pozi la pamoja kwenye zulia jekundu mwezi Agosti 2010.
Matt Damon
Kumbe Matt Damon anafanana na mama yake, Nancy! Cheki walivyopendeza wakati wa uzinduzi wa filamu ya Stuck on You mwezi Desemba 2003.
Matthew McConaughey
Matthew McConaughey akila pozi na mama yake, Mary, wakati wa uzinduzi wa filamu ya Two for the Money mwezi Septemba 2005.
Johnny Depp
Mama wa Johnny Depp , Betty Sue Palmer, alikuwa pembeni yake wakati wa uzinduzi wa filamu ya Nick of Time jijini Los Angeles mwezi Novemba 2005.
Jennifer Lawrence
Jennifer Lawrence akimkumbatia mama yake, Karen, kabla ya kupanda jukwaani kupokea tuzo yake ya Oscar mwezi Februari 2013.
Lena Dunham
Lena Dunham akimkumbatia kwa furaha mama yake, Laurie Simmons, wakati wa tuzo za Emmy mwezi Septemba 2013.
Halle Berry
Halle Berry na mama yake, Judith, wakiwa na tabasamu pana katika sherehe za Ebony 's Pre-Oscar Celebration mwezi Februari 2007.
Liam Hemsworth
Liam Hemsworth aliungana na mama yake mrembo, Leonie, wakati wa Kombe la Melbourne mwezi Novemba 2010.
Sarah Jessica Parker
Sarah Jessica Parker na mamaye, Barbra Forste, walihudhuria shoo ya Broadway Februari 2008.
Mary-Kate na Ashley Olsen
Mary-Kate na Ashley Olsen
walitunukiwa nyota kwenye orodha ya Hollywood Walk of Fame mwezi Aprili 2004
wakiwa na dada yao, Elizabeth; kaka yao, Trent; na mama yao, Jarnette.
Ben Affleck
Ben Affleck akiwa na mama yake, Chris, kwenye sherehe ya Jersey Girl jijini New York Machi 2004.
Ellen DeGeneres
Ellen DeGeneres na mamaye, Betty, wakiwa na tuzo wakati wa Tuzo za 32 za Daytime Emmy Awards mwezi Mei 2005 kwenye Ukumbi wa Radio City Music Hall jijini New York.
Justin Bieber
Justin Bieber na mamaye, Pattie, wakikumbatiana nje ya studio za Late Show mwezi Januari 2011.
Liv Tyler
Liv Tyler na mama yake, mwanamitindo wa zamani Bebe Buell, wakiwa wamekumbatiana wakati wa uzinduzi wa filamu jijini New York mwezi Juni 2011.
Heidi Klum
Heidi Klum na mamaye, Erna, wakila pozi wakati wa maonyesho ya tisa ya Victoria's Secret Fashion mwezi Novemba 2003.
Frank Ocean
Frank Ocean alikwenda na mamaye, Katonya Breaux Riley, kwenye chakula cha usiku cha Jarida la Time kutimiza miaka 100 (Time 100 Gala) jijini New York Aprili 2013.
Kate Middleton
Kate Middleton akiwasilia katika Hoteli ya The Goring akiwa na mama yake, Carole, na mdogo wake, Pippa Middleton, mwezi Aprili 2011.
Bradley Cooper
Bradley Cooper alikwenda na mamaye, Gloria Campano, kwenye sherehe za tuzo za Oscar mwezi Februari 2013.
Jake na Maggie Gyllenhaal
Jake na Maggie Gyllenhaal walikwenda na mama yao, Naomi Foner, kwenye uzinduzi wa filamu ya Moonlight Mile Septemba 2002 jijini Los Angeles.
Carrie Underwood
Mama wa Carrie Underwood , Carole, alikuwa pembeni yake kwenye Tuzo za CMA mwezi Mei 2006.
Molly Sims
Molly Sims na mama yake, Dorothy, waliketi mstari wa mbele kwenye shoo ya Diane von Furstenberg mwezi Februari 2008.
Rihanna
Rihanna akifurahia Tuzo yake ya American Music akiwa na mamaye, Monica Fenty, mwezi Novemba 2013.
Rachel Zoe
Wanamitindo Rachel Zoe na mamaye, Leslie Rosenweig, walikuwa pamoja jijini New York Septemba 2009 kwenye Usiku wa Mitindo (Fashion's Night Out).
Lily Collins
Lily Collins alikwenda na mamaye, Jill, kwenye uzinduzi wa filamu ya Abduction huko Hollywood mwezi Septemba 2011.
Melanie Griffith
Melanie Griffith na mamaye ambaye ni mwigizaji maarufu, Tippi Hedren, wakiwa wamependeza katika sherehe jijini Los Angeles mwezi Septemba 2012.
Salma Hayek
Salma Hayek na mamaye, Diana Jiménez Medina, wakiwa kwenye uzinduzi wa filamu ya Poseidon jijini Los Angeles mwezi Mei 2006.
Nina Dobrev
Wanavyofanana, kama maharage vile! Nina Dobrev na mamaye, Michaela, walihudhuria sherehe za jarida la Seventeen mwezi Mei 2012.
Zoe Kravitz
Zoe Kravitz akikumbatiana na mama yake, Lisa Bonet, kwenye uzinduzi wa filamu ya Conan the Barbarian jijini Los Angeles Agosti 2011.
Emma Stone
Emma Stone na mamaye, Krista, walihudhuria sherehe za mwaka 2012 za Tuzo za People's Choice kwenye ukumbi wa Nokia Theatre jijini Los Angeles Januari 2012.
Ryan Reynolds
Ryan Reynolds akiwa na mama yake, Tammy, kwenye uzinduzi wa filamu ya The Proposal huko Hollywood Juni 2009.
Selena Gomez
Selena Gomez akitabasamu katika pozi na mama yake, Mandy, kwenye ukumbi wa Vanity Fair wakati wa sherehe za Oscar jijini Los Angeles Februari 2012.
Vanessa Hudgens
Vanessa Hudgens na mamaye, Gina, waliwasili New York kushuhudia uzinduzi wa filamu ya Spring Awakening mwezi Agosti 2007.
Katherine Heigl
Katherine Heigl alikuwa na tabasamu pana na mamaye, Nancy, Oktoba 2008 kwenye ufunguzi wa duka la mitindo la Peter Alexander jijini Los Angeles.
Gwen Stefani
Gwen Stefani akimkumbatia mama yake, Patti, baada ya shoo yake ya LAMB Septemba 2005.
Julianne Hough
Julianne Hough akipigwa busu na mama yake,
Marriann Nelson, Julai 2011 kwenye fukwe za Miami.
Nicole Richie
Nicole Richie na mamaye, Brenda, wakiwa katika pozi kwenye sherehe ya Fox mwaka 2004.
Cate Blanchett
Cate Blanchett na mamaye, June, walinaswa laivu wakati wa sherehe za AFI Awards mwaka 2006.
Lindsay Lohan
Lindsay na mamaye Dina Lohan wakiwa katika pozi wakati wa sherehe ya kuzaliwa ya Lindsay alipotimiza miaka 21 Julai 2007.
Katy Perry
Katy Perry akimkumbatia mama yake, Mary Hudson, wakati wa uzinduzi wa albamu yake Juni 2008.
Sean Combs 'P.Diddy'
Sean "Diddy " Combs alikwenda na mama yake, Janice, kwenye sherehe za Tuzo za Emmy Septemba 2008.
George Clooney
Mama wa George Clooney , Nina Warren, aliongozana na mwanaye kwenye uzinduzi wa filamu ya Ocean's Twelve jijini Los Angeles Desemba 2004.
Jessica Alba
Jessica Alba na mamaye, Cathy, katika tukio mojawao Agosti 2005.
Colin Farrell
Colin Farrell aliongozana na mamaye, Rita, jijini Los Angeles kwenye uzinduzi wa filamu ya Miami Vice mwezi Julai 2006.
Kelly Osbourne
Kelly Osbourne akifurahia jambo na mama yake, Sharon, katika tukio moja Agosti 2011.
Paris Hilton
Paris Hilton alikuwa na mama yake, Kathy, wakati wa sherehe baada ya tuzo za Golden Globes Januari 2012.
No comments:
Post a Comment