Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama
na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali
ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi
jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye
anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za
nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi,
Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30,
wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka
JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya
Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya
Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar
es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa
Shahada hiyo hapo chuoni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika mahafali ya
Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi
jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30
wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa
umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na
idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka nchi za nje ambazo
ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya
kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha
Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26,
2014
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na wahitimu wa Kozi ya
Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar
es salaam leo Julai 26, 2014
No comments:
Post a Comment