Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 10 July 2014

HAYA YA BRAZIL KUPIGWA 7-1 NI MAJANGA, KWA SIMBA SC MUDA WA KUPANGA MAJESHI UMEFIKA, FANYENI HAYA…….

_DSC0648Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
LUIZ Felipe Scolari amekubali kubeba lawama zote kutokana na fedheha waliyoipata Brazil kutoka kwa `watu katili` Ujerumani.
Haikutegemewa na wengi kama Brazil wangeingia katika rekodi mbaya ya kombe la dunia kwa kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia jana usiku.
Brazil waliojiamini, waliingia kwa kasi, lakini bao la mapema la Thomas Muller liliwatoa upepo ghafla ya kufungisha mabao mengi zaidi.
Bora Neymar hakuwepo katika mchezo huo. Huyu ni mchezaji mwenye kiwango cha juu kama alivyo kwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Kama angekuwepo uwanjani, halafu Brazil ikafungwa mabao kama ya jana, basi ingemharibu zaidi katika maisha yake ya soka.
Tatizo kubwa la Brazil lilikuwa kwenye safu ya ulinzi iliyoongozwa na nahodha David Luiz, Maicon, Marcelo na Dante. Hawa walikuwa tatizo jana, walikaba vibaya, utulivu ulikuwa `F`. Hata Neymar angekuwepo, kwa aina ya uchezaji wake, bado safari ya Brazil ingefika mwisho kwasababu asingekuwa na jinsi ya kuwaokoa.
article-2685267-1F7E09A000000578-454_634x476Mambo ya `wedi kapu` haya, si mchezo: David Luiz alishindwa kuzuia machozi baada ya `mbungi` kumalizika.
Pole sana Scolari, pole sana Neymar, Pole sana Thiago Silva, pole sana wananchi wa Brazil, pole sana mashabiki wa Brazil duniani kote. Huo ndio mpira wa miguu, Rekodi yenu itazungumzwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
Hongereni Ujerumani kwa ushindi mnono. Hongereni kwa Miroslav Klose kuvunja rekodi ya gwiji wa Brazil, Ronaldo. Mabao 16 na kuwa mfalme wa mabao wa kombe la dunia ni heshima kubwa.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment