Mbunge wa Tabora Mjini aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage, akionyesha bastola kiunoni huko Igunga mwaka 2011.
Ismail Aden Rage akiongoza mapambano na wanaCCM wenzake dhidi ya wafuasi wa Chadema mjini Dodoma wakigombea kusimika bendera ya tawi.
Na Hastin Liumba, Tabora
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya Tabora mjini kimetoa matokeo ya awali ya wagombea ubunge ambapo hadi sasa mbunge Ismail Aden Rage ameanguka vibaya.
Akitangaza matokeo hayo katibu wa CCM wilaya ya Tabora Mjini, Kanuth Ndaghine, alisema anatoa matokeo hayo ya awali taarifa kamili atatoa kesho mara baada taarifa kutoka Kata ya Kiloleni.
Ndaghine alisema hadi sasa katika matokeo hayo ya awali mgombea Emmanuel Mwakasaka anaongoza kwa kura 11,280 na mbunge ambaye alikuwa akitetea jimbo hilo Ismail Aden Rage kura 3,380.
Katibu huyo alisema matokeo hayo yatakamilika baada ya kasoro za karatasi zitakapohakikiwa katika baadhi ya kata kama vile Ntalikwa.
Katika jimbo la Igalula mtoto waziri wa zamani wa Ardhi na nyumba Tatu Ntiumizi,Musa Ntimizi anaongoza kwa kura 7,200 kwa akifuatiwa na mbunge ambaye alikuwa akitetea jimbo hilo Dk Athuman Mfutakamba kura 3,500 na Hanifa Kitwana Kondo kura 3,200 ambapo kura hizo bado zinajumlisha.
Jimbo la Tabora Kaskazini mbunge aliyekuwa akitetea jimbo lake Shafin Mamlo Sumar kura 6,000 Joseph Kidaha 5,000 baada ya Almas Maige 9,000 kuonyesha anaongoza kwa kura nyingi.
Jimbo la Ulyankulu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua John Kadutu 13,600 Dk Msonde Sdyen 1,167 ila bado matokeo halisi ,huku Profesa Kapuya kuna kitu kinaitwa Sintofahamu.
Jimbo la Urambo Mashariki mke wa spika wa zamani Samwel Sitta, Magreth Sitta anaongoza kwa kuzoa kura 12,392 dhidi ya Ali Maswanya mwenye kura 4,175.
Aidha jimbo jipya la Manonga Seif Gulamali anaongoza hadi sasa matokeo yake bado ambapo katibu wa CCM Abdallah Kazwika hajapatikana kutoa taarifa ya jimbo hilo,huku jimbo la Bukene Suleiman Zedi 12,894 Deo Kahumbi 2,728,Tedy Kaselabantu 1,441 ambapo jimbo la Sikonge mbunge Said Nkumba anaongoza dhidi ya mgombea Rajab Kakunda.
Jimbo la Nzega Mjini Husein Bashe anaongoza akifuatiwa na Joseph Ngulumwa, huku Dk Hamis Kingwangala anaongoza jimbo la Nzega Vijijini akifuatiwa na mbunge wa zamani Lucas Selelii.
No comments:
Post a Comment