Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 2 August 2015

ARSENE WENGER AMFUNGA MOURINHO, ARSENAL YABEBA NGAO YA JAMII

Chamberlain
Mabingwa wa kombe la FA Arsenal wameshinda kombe la Charity Shield kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuwashinda mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea 1-0 katika Uwanja wa Wembley.

Alex Oxlaide Chamberlain alifunga bao hilo la ushindi na mguu wake wa kushoto na kumfanya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, afurahie ushindi wake dhidi ya Jose Mourinho wa Chelsea.
Ramires alishindwa kufunga bao la wazi kutoka krosi iliopigwa na Loic Remy huku Chelsea ikishindwa kuona lango la wapinzani wake kabla ya muda wa mapumziko.
Mourinho
Eden Hazard alipiga juu ya goli alipokuwa amesalia na kipa kabla ya mkwaju uliopgwa na Oscar kutolewa nje na kipa Petr Cech.
Ni mara ya kwanza kwa kipa huyo wa zamani wa Chelsea kuokoa hatari baada ya dakika 68 kabla ya kuokoa kichwa cha Kurt Zouma.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment