Bunge la Kenya.
Wakenya wanakabiliwa
na tisho la kufungwa jela mwaka mmoja au kulipa faini ya dola 23,000 kwa kukosa
kumuita mbunge 'mheshimiwa' unapozungumza naye.
Sheria hii mpya
inayopendekezwa na wabunge wa Kenya inalenga kuhakikisha kila afisa mkuu wa
serikali anapewa heshima anayostahili.
Watakaovunja sheria
hiyo watapata adhabu kali.
Adhabu hiyo itawakuta wale watakaokosa kumpa
Rais heshima zake kwa kumuita 'Mtukufu Rais', naye spika wa bunge atapaswa
kuitwa 'Mheshimiwa spika wa bunge'
Mswada huu
uliwasilishwa na mbunge mmoja kwa jina Adan Keynan, ambaye amesema kuwa umuhimu
wake ni kuonyesha heshima kwa maafisa wa serikali.
"ni muhimu
kuonyesha picha nzuri ya nchi, kuhakikisha kuna mpangilio na maadili mema
katika mchakato wa utawala, '' alisema bwana Keynan.
Huku mzozo kati ya
wabunge na magavana ukiendelea kutokota, mswada huo haujapendekeza chochote
kuhusu cheo cha magavana ambao ni wakuu wa majimbo na watakavyoitwa.
Wataendelea kuitwa tu
magavana.
Mswada huo pia
unapendekeza kuwepo vyeo kwa maafisa wa serikali kulingana na ukubwa wao.
Ikiwa mswada huo
utakuwa sheria, cheo cha mbunge kitakuwa juu zaidi kuliko cha gavana , majaji
wa mahakama ya juu , marais wa zamani na makamu wa rais.
Kadhalika mswada huo
utatumika katika kuweka mpangilio kuhusu ambavyo maafisa wa serikali watakuwa
wanaketi katika hafla na mikutano ya serikali.
Maafisa wa serikali
watakaojipatia vyeo vingine mbali na vile vitakavyoorodheshwa katika mswada huo
watatowa faini ya dola milioni mbili.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment