VURUGU ilizotokea nje ya Uwanja wa Anfield kufuatia Liverpool kufungwa na Chelsea mabao 2-0 jana.
Picha zinaonyesha kitimutimu cha maana nje ya Uwanja wa Anfield Road baada ya mashabiki wa Liverpool kuwavaa mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakiimba jina la Nahodha wa Wekundu hao, Steven Gerrard baada ya mechi.
Shabiki mmoja alitupa konde kwa mwenzake, wakati wengine walitenganishwa na Polisi.
Makosa ya Gerrard yalisababisha bao la kwanza la Chelsea lililofungwa na Demba Ba na mashabiki wa The Blues wakawatia hasira Liverpool kwa kuimba jina la mchezaji huyo.

Wawili tu: Mashabiki wakizipiga chanzo ni kuzomewa kwa Steven Gerrard

Polisi wakituliza ghasia

Sio salama: Baba akiongozana na kijana wake kutoka eneo la vurugu huku watu wakiendelea kuchapana nyuma yake

Ilikuwa si mchezo: Polisi walilazimika kuwaachanisha watu wengine waliopelekana hadi chini katika mapambano yao

Wakorofi: Polisi wakiwwka uzio baina ya mashabiki wa Liverpool na Chelsea

Waacheni tuwachape: Mashabiki wa Liverpool wakisema na Polisi waliokuwa wakituliza ghasia hizo
CHANZO MPENJA BLOG


No comments:
Post a Comment