
Maandamano
kuhusu wasichana waliotekwa
Maandamano makubwa ya kwanza yanatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Nigeria- Abuja baadaye leo watu wakiitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwanusuru wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislam .
Wasichana
hao walichukuliwa kutoka shule yao ya malazi iliyopo katika eneo lisiloweza
kufikiwa kwa urahisi kaskazini mashariki mwa nchi zaidi ya wiki mbili
zilizopita.
Waandalizi
wa maandamano hayo wanaita serikali kuelekeza juhudi zao kwa wasichana
waliopotea .
Mpango
ni kuandamana hadi bungeni na kwa mshauri wa taifa wa masuala ya usalama na
kuwasilisha barua ya kutoa wito wa kufanyika kwa juhudi zaidi kuwanusuru
wasichana hao.
Mwanaharakati
mmoja wa kijamii amesema katika nchi nyingine yoyote ile suala la kutekaji
nyara wa wasichana hao wengi lingekuwa ni mjadala wa kila siku .
Lakini
serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kukaa kimwa huku
wazazi wenye shauku wakisailia kuwa gizani kuhusu nini kinachoendelea kuhusiana
na wasichana wao.
Huenda
kwa kuhisi hilo rais wa Seneti , David Mark, sasa amezungumza. Amewatolea wito
watekaji kuawaachilia mara moja wasichana bila masharti na akasema bila shaka
taifa letu liko vitani .
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment