
Swala a tata la ubaguzi wa rangi katika
michezo limeibua mchango wa rais wa Brazil.
Rais Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa kimataifa wa Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na tukio la ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga kati ya Barcelona na Villareal .
Mchezaji huyo wa Barcelona
aliokota ndizi aliyokuwa ametupiwa na kuila kabla ya kuitupa na kuendelea na
mchezo.
Bi Rousseff aliandika katika
mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na
ubaguzi wa rangi katika kandanda na kuwa ni tukio la kuigwa .
Klabu ya Villarreal inasema
kuwa imempiga marufuku mwanaume ambaye alitupa ndizi hiyo uwanjani na kuwa
hatohudhuria mechi zote za nyumbani za klabu hiyo maishani.
Mamia ya watu na wachezaji
maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao
kwenye mitandao wa kijamii wakila ndizi.
Mchezaji wa Manchester City
Sergio Aguero alipachika picha akila ndizi sawa na nyota ya soka ya wanawake
Marta, wengine ni Luiz Suarez wa Liverpool,Oscar, David Luiz na Willian wote wa
Chelsea .
Rais wa Fifa sepp Blatter
ameongezea sauti yake katika tukio la hivi punde akisema ni vibaya kwa dhulma
hizo kuendelea katika karne hii.

Sergio Aguero (kushoto) akila ndizi kupinga kitendo hicho


Neymar (kushoto) akila ndizi kuashiria kuwa anapinga kitendo hicho, kulia ni mchumba wa Daniel Alves (aliyebaguliwa) akiwa ameshika ndizi.

Mtangazaji wa televishen Marilo Montero akila ndizi kuonesha kuwa anapinga ubaguzi

wacheazaji wa Totenham, Mousa Dembele na Nacer Chadli wakila ndizi kupiga kitendo hicho

Hulk pia alipinga kitendo hicho cha ubaguzi wa rangi

Coutinho na Suarez nao walikula ndizi kupinga ubaguzi

Bacary Sagna alionekana akila ndizi kupinga kitendo hicho

Fernadinho akiwa na mwanae wote walikuwa wakila ndizi kupinga ubaguzi huo.
No comments:
Post a Comment