Safari kunako mashakani: Raia wa Sudan Kusini wakikimbia machafuko katika mji wa Bentiu.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafikiria kuweka vikwazo dhidi ya makundi yanayopigana nchini Sudan Kusini, huku rais wa nchi hiyo Salva Kiir, akimfukuza kazi mkuu wa majeshi, baada ya waasi kuutwa mji wa Bentiu.
Mkuu wa shughuli za
kulinda amani za Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous na msaidizi wa katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binaadamu, Ivan Simonovic, wamewapa
maelezo mafupi wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali
ya kusambaa kwa mashambulizi ya raia, yakiwemo mauaji ya kikabila kwenye mji wa
Bentui wenye utajiri wa mafuta pamoja na mauaji ya watu kadhaa walioomba
hifadhi kwenye kambi ya kikosi cha kulinda amani cha umoja huo kilichoko mjini
Bor.
Ladsous amesema mauaji ya
raia wasio na hatia yataendelea iwapo pande zinazopigana hazitoweka chini
silaha na kujikita zaidi katika mazungumzo yenye kuleta tija. Amesema Umoja wa
Mataifa unafanya kila uwezalo, kuwalinda raia wanaokimbia vita, lakini ikumbukwe
kuwa jukumu la kwanza la kuwalinda raia liko mikononi mwa serikali. Ladsous
ameonya kuwa vita hivyo vinaweza kuwa janga la kibinaadamu, iwapo
havizasitishwa.
Wanachama waunga mkono
vikwazo
Balozi wa Nigeria kwenye
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Joy Ogwu, ambaye ndiyee rais wa baraza
hilo kwa mwezi huu wa Aprili, amesema wanachama wanaunga mkono vikwazo kuwekwa
dhidi ya Sudan Kusini.
Tayari Marekani na Umoja
wa Ulaya zimetishia kuiwekea vikwazo Sudan Kusini. Mwanzoni mwa mwezi huu, Rais
Barack Obama aliidhinisha vikwazo kadhaa dhidi ya wale wote wanaohusika na
kukiuka haki za binaadamu Sudan Kusini au kudhoofisha demokrasia na kuzuia
mchakato wa amani.
Mkuu wa majeshi atimuliwa
Wakati hayo yakijiri,
Rais Salva Kiir amemfukuza kazi mkuu wa majeshi wa Sudan Kusini, Jenerali James
Hoth Mai na nafasi yake kuzibwa na Jenerali Paul Malong. Hata hivyo, sababu za
kufukuzwa hazijatangazwa, ingawa duru za karibu zinaeleza kuwa huenda sababu
ikawa kushindwa kwa jeshi kuudhibiti mji wa Bentiu ulioko kaskazini mwa nchi
hiyo.
Rais Kiir pia amemfukuza
kazi mkuu wa ujasusi, Jenerali Paul Mach na nafasi yake kuchukuliwa na Jenerali
Marial Nour Jok. Jeshi la Sudan Kusini limekuwa likipigana na waasi tangu
Disemba 15 mwaka uliopita, lakini mzozo huo umegeuka na kuwa wa kikabila kati
ya kabila la Kiir la Dinka na kabila la Nuer, la kiongozi wa waasi, Riek
Machar.
Wakati huo huo, kikosi
cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusiniu, kimeishutumu
serikali ya nchi hiyo kwa kueneza taarifa za uongo kwamba kambi ya umoja huo
karibu na eneo yalipotokea mauaji, ilikataa kuwahifadhi wahanga.
Shirika
la kimataifa la haki za binaadamu la Human Rights Watch, limelitaka Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya Bentiu na vifo vingine
vilivyotokea mwanzoni mwa mwezi huu kwenye mji wa Bor.
CHANZO, DW.DE.COM/SWAHILI
No comments:
Post a Comment