Generali James Hoth Mai amefutwa kazi na Salva Kiir ingawa Rais huyo hajatoa sababu ya hatua yake.
Amri iliyotolewa na
Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa
katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr
hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo, nchi hiyo imekuwa
ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba, wiki jana waasi
waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja
wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa
serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika
mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje
wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari
kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa
walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka
mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa
wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi
ya ukabila.
Hata hivyo waasi
wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN
kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio
katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment