Rais Obama amewasili
Korea Kusini huku hofu ikizagaa kwamba Korea Kaskazini huenda inajiandaa
kufanya jaribio la nne ya zana zake za nukyla.
Inatarajiwa kwamba
shughuli mpya katika kinu cha nuklya mjini Pyongyang zitatawala mazungumzo kati
ya bwana Obama na rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.
Viongozi hao wawili
wanarajiwa kuangazia zaidi jukumu la Uchina katika kuithibiti Korea Kaskazini,
jambo ambalo Bwana Obama ametaja kuwa lenye umuhimu mkubwa.
Rais wa Marekani
Barack Obama amewasili Korea Kusini katika sehemu yake ya pili ya ziara katika
Bara la Asia. Anatarajiwa kukutana na Rais Park baadaye leo na kuwatembelea
wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo.
Ziara yake inafanywa
wakati ambapo kuna hofu kuwa Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio la nne la
Kinukilia.
Korea Kaskazini
inatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao wawili na tayari kuna ripoti kuwa
maandalizi ya kufanya jaribio la Kinukilia yanayoendelea kufanywa Korea
Kaskazini yatahakikisha kuwa taifa hilo jirani linapewa kipao mbele katika
mashauriano.
Picha zilizochukuliwa
na mitambo ya Sattelite zinaonyesha kuwa kuna masanduku mengi yanayohamishwa
hapa na pale katika eneo linalotarajiwa kufanyiwa zoezi hilo Korea Kaskazini.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment