Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John
Kerry akizungumza na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Waziri wa Mashauri ya
Kigeni wa Marekani amelaumu Urusi kwa kuchochea mapigano Mashariki mwa Ukraine.
John Kerry alisema
ujasusi wa Marekani una hakika kuwa Urusi imetoa silaha na wapiganaji na pia
inaendelea kugharamia na kusimamia wapiganaji wa nchini Ukraine kushiriki
ghasia hizo.
Katika lugha ya
hasira, Bwana Kerry, alishambulia Urusi akisema kuwa taifa hilo limeshindwa
kuchukua hatua madhubuti za kujaribu kutuliza uhasama ulioko nchini Ukraine
kama ilivyokubaliwa mjini Geneva juma lililopita.
Bwana Kerry alisema
kuwa Urusi inasimamia ghasia zinazoendeshwa na watu wanaotaka kujitenga kutoka
kwa Ukraine Mashariki mwa taifa hilo na kujaribu kusababisha ghasia ili
kuhujumu uchaguzi unaotazamiwa kufanywa mwezi ujao.
Kwa hasira, Bwana
Kerry alilaumu Urusi kwa ghasia zote zinazoendelea Ukraine wakati huu. Ingawa
hakutangaza vikwazo inavyoweza kuongezewa Urusi Bwana Kerry alisema mwanya wa
kuimarisha amani katika Ukraine unaendelea kuziba.
CHANZO, BBCSWAHILI.
No comments:
Post a Comment