Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 13 August 2015

WABUNGE 336 WA CCM HAWA HAPA, DK. KABOUROU YULEEEE!


Na Daniel Mbega
HATIMAYE kitendawili kimeteguliwa. Chama cha Mapinduzi leo hii kimeweka hadharani majina ya wabunge wake watarajiwa 336 baada ya kupitishwa na Halmashauri Kuu (NEC) huku wanasiasa walitoka upinzani na ‘kupotea’ safari hii wakirejea tena ulingoni.
Miongoni mwao yumo mwanasiasa aliyepata kuteka ulingo wa siasa wa Tanzania na kuwa mbunge wa kwanza wa upinzani kabla ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi. Huyu si mwingine bali ni Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Walid Amani Kabourou, ambaye akipitishwa kuwania Jimbo ‘lake’ la Kigoma Mjini alilolipoteza mwaka 2005 kwa Peter Serukamba wa CCM.
Ukimuacha Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, hapana shaka yoyote kwamba Dk. Walid Amani Kabourou ndiye mwanasiasa wa upinzani aliyeitetemesha nchi na ndiye alikuwa mbunge wa kwanza kutoka upinzani mwaka 1994 wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chadema, enzi hizo Edwin Mtei akiwa Mwenyekiti.
Itakumbukwa kwamba, Dk. Kabourou (66) alikuwa akipelekeshana na mpinzani wake mkubwa Azim Premji ‘Maghorofani’ ambapo walianza kunyang’anyana ushindi kupitia mahakama na mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu akashinda tena hadi mwaka 2005 alipoangushwa na Peter Serukamba wa CCM.
Dk. Kabourou, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema kabla ya kumpisha Dk. Wilbrod Slaa, atakumbukwa jinsi alivyokuwa akichukuliwa kama ‘mfalme’ wa Kigoma mjini kiasi kwamba kuna wakati wananchi walimbeba kwenye machela kama walivyokuwa wakiwabeba wakoloni!
Hata hivyo, mwaka 2006 akaamua kujiunga na CCM na duru za siasa zinamtuhumu kwamba ‘alitumiwa’ na chama hicho tawala kuua upinzani kabla ya kupewa ‘fadhila’ ya ubunge wa Afrika Mashariki mwaka 2007.
Mwaka 2010 hakuambua kitu, lakini mwaka 2012 akawania uenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma na kumbwaga hasimu wake wa siku nyingi, Azim Premji ‘Maghorofani’, cheo ambacho anacho mpaka sasa. Mvuto wake kisiasa si kama ule wa kwanza na ashukuru tu kwamba Peter Serukamba amekimbilia Kigoma Kaskazini kwa Zitto Kabwe.
Ukiacha Dk. Kabourou, yumo pia Daniel Nsanzugwanko ambaye anagombea Kasulu Mjini badala ya Kasulu Mashariki. Mwanasiasa huyo aliyekuwa NCCR-Mageuzi kabla ya kurudia CCM mwaka 2000, alikuwa ametoweka ulingoni.
Aliingia Bungeni kupitia CCM mwaka huo wa 2000 baada ya kushinda katika Jimbo la Kasulu Mashariki ambalo alilitafuta mwaka 1995 akalikosa.
Kampeni zake za kura za maoni mwaka 2000 zilikumbwa na utata baada ya mbunge wa jimbo hilo Teddy Magayane kufariki ghafla na kifo chake kuhusishwa na imani za kishirikina.
Nsanzugwankwo alibahatika kuwa Naibu Waziri katika Awamu ya Nne akishika wadhifa huo katika Wizara ya Kazi na Ajira na baadaye Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Hata hivyo, mwaka 2010 aliangukia pua kwenye uchaguzi mkuu baada ya kushindwa na Zaituni Agripina Buyogela wa NCCR-Mageuzi na hata rufaa yake kupinga matokeo hayo nayo ikatupiliwa mbalina Mahakama Kuu mwaka 2013.
Wagombea ubunge wengine ambao wamerejea ulingoni ni George Malima Lubeleje wa Mpwapwa ambaye mwaka 2010 aliangushwa na Gregory Teu; Vedasto Mathayo Manyinyi wa Musoma Mjini ambaye mwaka 2010 aliangushwa na Vincent Kiboko Nyerere wa Chadema; Dk. Diodorus Buberwa Kamala anayewania tena jimbo la Nkenge; Suleiman Ahmed Saddiq ‘Murad’ ambaye amerejea Mvomero baada ya kumwangusha Naibu Waziri wa Maji Amos Makala ambaye alimnyang’anya kiti hicho mwaka 2010.

HAWA NDIO WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA MAJIMBO NA VITI MAALUM KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2015

1. Arusha
Arusha: Mjini Philemon Mollel
Karatu: Dkt. Wilbard Slaa Lorri
Arumeru Magharibi: Loy Thomas ole Sabaya
Arumeru Mashariki: John Danielson Sakaya (JD)
Longido: Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa
Monduli: Namelock Edward Sokoine
Ngorongoro: William Tate ole Nasha

2. Dar es Salaam
Ukonga: KURA ZINARUDIWA
Ilala: Zungu Mussa Azzan
Segerea: Bonna Mosse Kaluwa
Temeke: Abasi Zuberi Mtemvu
Kigamboni: Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile
Mbagala: Issa Ally A. Mangungu
Kawe: Kippi Ivor Warioba
Ubungo: Dkt. Didas John Masaburi
Kibamba: Dkt. Fenela E. Mkangala
Kinondoni: Iddi Azzan

3. Dodoma
Chemba: Juma Selemani Nkamia
Bahi: Omar Ahmed Badwel
Kibakwe: George Boniface Simbachawene
Mpwapwa: George Malima Lubeleje
Mtera: Livingstone Joseph Lusinde
Chilonwa: KURA ZINARUDIWA
Dodoma: Mjini Antony Peter Mavunde
Kongwa: Job Y. Ndugai
Kondoa Mjini: Sanda Edwin
Kondoa Vijijini: Dkt. Ashatu Kijaji

4. Geita
Geita Mjini: Costantine John Kanyansu
Geita Vijijini: Joseph Lwinza Kasheku
Busanda: Lolensia Masele Bukwimba
Mbogwe: Augustino Manyanda Massele
Bukombe: Doitto Mashaka Biteko
Chato: Dkt. Medard Matogolo Kalemani
Nyang’hwale: Hussein Nassor Amar

5. Iringa
Iringa Mjini: Mwakalebela Fredrick Wilfred
Isimani: William Vangimembe Lukuvi
Kalenga: Godfrey William Mgimwa
Kilolo: KURA ZINARUDIWA
Mufindi Kaskazini: Mahmoud Hassan Mgimwa
Mufindi Kusini: Mendrad Lutengano Kigola
Mafinga Mjini: Cosato David Chumi

6. Kagera
Bukoba Mjini: Balozi Khamis Sued Kagasheki
Bukoba Vijijini: Jasson Samson Rweikiza
Biharamulo: Osca Rwegasira Mkassa
Karagwe: Innocent Luugha Bashungwa
Kyerwa: Innocent Sebba Bilakwate
Muleba Kaskazini: Charles John Mwijage
Muleba Kusini: Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka
Nkenge: Diodorus Buberwa Kamala
Ngara: Alex Raphael Gashaza

7. Katavi
Mpanda Mjini: Sebastian Simon Kapufi
Mpanda Vijijini: Moshi Selemani Kakoso
Katavi: Issack Aloyce Kamwele
Nsimbo: Richard Philip Mbogo
Kavuu: Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe

8. Kigoma
Buyungu: Eng. Christopher K. Chiza
Muhambwe: Eng. Atashasta Nditye
Kasulu Mjini: Daniel Nsanzugwanko
Kasulu Vijijini: Augustino Vuma Holle
Manyovu: Albert Obama Ntabaliba
Kigoma Mjini: Dk. Amani Walid Kabourou
Kigoma Kaskazini: Peter Joseph Serukamba
Kigoma Kusini: Hasna Sudi Mwilima

9. Kilimanjaro
Hai: Danstan Lucas Mallya
Siha: Aggrey Deaidile Mwanri
Moshi Mjini: Mosha Davis Elisa
Mwanga: Profesa Jumanne A. Maghembe
Same Mashiriki: Anne Kilango Malecela
Same Magharibi: David Mathayo David
Moshi Vijijini: Dkt. Cyril August Chami
Vunjo: Innocent Melleck Shirima
Rombo: Sanje Samora Colman

10. Lindi
Ruangwa: Majaliwa Kassim Majaliwa
Liwale: Faith Mohamed Mitambo
Nachingwea: Hassan Elias Masala
Mtama: Nape Moses Nnauye
Mchinga: Said Mohamed Mtanda
Lindi Mjini: Hassan Seleman Kaunje
Kilwa Kusini: Hasnain Gulamabas Dewji
Kilwa Kaskazini: Murtaza Ally Mangungu

11. Mara
Bunda Mjini: Steven Masatu Wasira
Mwibara: Kangi Alphaxard Lugola
Bunda Vijijini: Boniface Mwita Getere
Tarime: Christopher Ryoba Kangoye
Tarime Mjini: Michael Mwita Kembaki
Serengeti: Dkt. Steven Kebwe Kebwe
Butiama: Nimrod Elirehemah Mkono
Butiama Vijijini: Prof. Sospeter Mwinjarubi Muhongo
Rorya: Lameck Okambo Airo
Musoma Mjini: Vedastus Mathayo Manyinyi

12. Manyara
Babati Mjini: Kisyeri Chambiri
Babati Vijijini: Jittu Vrajilal Son
Hanang’: Dkt. Mary Michael Nagu
Kiteto: Litaamuliwa na Kikao Kijacho cha Kamati Kuu
Mbulu Mjini: Zacharia Paulo Issaay
Mbulu Vijijini: Fratei Gregory Massay
Simanjiro: Christopher Olonyhokie Ole Sendeka

13. Mbeya
Mbeya Mjini: Sambwee Shitambala Mwalyego
Mbeya Vijijini: Oran M. Njeza
Mbarali: Haroon Mullah Pirmohamed
Rungwe: Sauli Henry Amon
Busokelo: Atupele Fredy Mwakibete
Ileje: Janeth Zebedayo Mbene
Mbozi: Weston Godfrey Zambi
Vwawa: Ngailonga Josephat Kasunga
Momba: Dk. Luca Jelas Siyame
Tunduma: Frank Mastara Sichalwe
Lupa: Victor Mwambalaswa
Songwe: Philip A. Mulugo
Kyela: Dkt. Harrison George Mwakyembe

14. Morogoro
Morogoro Mjini: Abood Mohamed Abdul Aziz
Morogoro Kusini: Prosper Joseph Mbena
Morogoro Kusini Mashariki: Omar Tibweta Mgumba
Gairo: Ahmed Shabiby
Mvomero: Suleiman Ahmed Saddiq
Mikumi: Jones Estomih Nkya
Kilombero: Abubakar Damian Asenga
Mlimba: Godwin Emmanuel Kunambi
Ulanga Mashariki: Celina Ompeshi Kombani
Ulanga Magharibi: Dkt. Hadji Mponda
Kilosa: Mbaraka Salum Bawazir

15. Mtwara
Mtwara Mjini: Hasnen Mohamed Murji
Nanyamba: Abdallah Dadi Chikota
Mtwara Vijijini: Hawa Abdulhaman Ghasia
Tandahimba: Shaibu Salum Likumbo
Newala: George Huruma Mkuchika
Newala Vijijini: Rashid Ajali Akbar
Nanyumbu: William Dua Mkurua
Ndanda: Mariam Reuben Kasembe
Masasi: Chuachua Mohamed Rashid
Lulindi: Jerome Dismas Bwanausi

16. Mwanza
Ilemela: Angelina Sylvester Lubala Mabula
Nyamagana: Stanslaus S. Mabula
Kwimba: Mansoor Shanif Hiran
Sumve: Richard Maganga Ndassa
Misungwi: Charles Mhangwa Kitwanga
Magu: Boniventura Desdery Kiswaga
Sengerema: William Mganga Ngeleja
Buchosa: Dkt. Charles John Tzeba
Ukerewe: Christopher Nyandiga

17. Njombe
Njombe Kaskazini: Joram Hongoli
Njombe Kusini: Litaamuliwa na Kikao Kijacho cha Kamati Kuu
Makambako: Deo Kasenyenda Sanga
Wanging’ombe: Gerson Hosea Lwenge
Ludewa: Deo Filikunjombe
Makete: KURA ZINARUDIWA

18. Pwani
Bagamoyo: Dkt. Shukuru Kawambwa
Chalinze: Ridhiwani J. Kikwete
Kibaha Mjini: Sylvester Francis Koka
Kibaha Vijijini: Hamoud Abuu Jumaa
Kisarawe: Selemani Said Jaffo
Mafia: Mbaraka K. Dau
Mkuranga: Abdallah H. Ulega
Rufiji: KURA ZINARUDIWA
Kibiti: Ally Seif Ungando

19. Rukwa
Sumbawanga Mjini: Aeshi Khalfan Hilaly
Nkansi Kaskazini: Ally Mohamed Kessy
Nkansi Kusini: Deuderit John Mipata
Kwela: Ignas Aloyce Malocha
Kalambo: Josephat Sinkamba Kandege

20. Ruvuma
Songea Mjini: Leonidas Tutubert Gama
Nyasa: Eng. Stella Martin Manyanya
Tunduru Kaskazini: Ramo Matala Makani
Tunduru Kusini: Daimu Iddi Mpakate
Peramiho: Jenister Joakim Mhagama
Madaba: Joseph Kisito Mhagama
Namtumbo: KURA ZINARUDIWA
Mbinga Mjini: Sixtus Raphael Mapunda
Mbinga Vijijini: KURA ZINARUDIWA KATA MBILI

21. Simiyu
Bariadi: Andrew John Chenge
Itilima: Njalu Daudi Silanga
Meatu: Salum Khamis Salumu
Kisesa: Luhanga Joelson Mpina
Busega: KURA ZINARUDIWA
Maswa Mashariki: Stanslaus Haroun Nyongo
Maswa Magharibi: Mashimba Mashauri Ndaki

22. Singida
Singida Mjini: Ramadhani Sima
Singida Kaskazini: Lazaro Nyalandu
Iramba Mashariki: Joseph Allan Kiula
Iramba Magharibi: Mwigulu Lamech Nchemba
Manyoni Magharibi: Yahya Omari Masare
Manyoni Mashariki: Daniel Edward Mtuka
Singida Mashariki: Litaamuliwa na Kikao Kijacho cha Kamati Kuu
Singida Magharibi: Elibariki Emmanuel Kingu

23. Shinyanga
Shinyanga Mjini: Steven Masele
Solwa: Ahmed Ally Salum
Kishapu: Suleiman Masoud Nchambi
Msalala: Ezekiel Magolyo Maige
Ushetu: Elias John Kwandikwa
Kahama Mjini: Kishimba Jumanne Kibera

24. Tabora
Tabora Mjini: Emmanuel Mwakasaka
Igalula: Ntimizi Rashidi Mussa
Uyui: Maige Athumani Almas
Sikonge: George Joseph Kakunda
Urambo: Margareth Samwel Sita
Kaliua: Profesa Juma Athuman Kapuya
Ulyankulu: John Peter Kadutu
Nzega Mjini: Hussein Mohamed Bashe
Bukene: Suleiman Juma Zedi
Nzega Vijijini: Dkt. Hamis Andrea Kigwangala
Igunga: Dkt Dalaly Peter Kafumu
Manonga: Seif Hamis Said

25. Tanga
Tanga Mjini: Omari Rashid Nundu
Lushoto: Shabani Omari Shekilindi
Bumbuli: Januari Yusuf Makamba
Mlalo: Rashid Abdallah Shangazi
Pangani: Jumaa Hamidu Aweso
Kilindi: Omari Mohamed Kigua
Mkinga: Danstan Luka Kitandula
Handeni Mjini: Dkt. Abdallah Omar Kigoda
Handeni Vijijini: Mboni Mohamed Mhita
Muheza: Balozi Adadi Mohamed Rajabu
Korogwe Mjini: Mary Pius Chatanda
Korogwe Vijijini: Stephen Hillary Ngonyani

1. Kaskazini Pemba
Gando: Salim Bakar Issa
Kojani: Masoud Ali Moh’d
Mgogoni: Issa Juma Hamad
Mtambwe: Khamis Seif Ali
Wete: Dkt. Abdalla Saleh Abdalla
Micheweni: Khamis Juma Omar
Tumbe: Rashid Kassim Abdalla
Konde: Ramadhan Omar Ahmed
Wingwi: Khamis Shaame Hamad

2. Kaskazini Unguja
Chaani: Khamis Yahya Machano
Kijini: Makame Mashaka Foum
Mkwajuni: Khamis Ali Vuai
Nungwi: Mustafa Makame Hamadi
Tumbatu: Juma Othman Hija
Bumbwini: Mbarouk Juma Khatib
Donge: Sadifa Juma Khamis
Kiwengwa: Khamis Mtumwa Ali
Mahonda: Bahati Ali Abeid

3. Kusini Pemba
Chake Chake: Mbaraka Said Rashid
Chonga: Abdalla Omar Muya
Ole: Omar Mjaka Ali
Wawi: Daud Khamis Juma
Ziwani: Mohamed Othman Omar
Chambani: Moh’d Abdulrahman Mwinyi
Kiwani: Rashid Abdulla Rashid
Mkoani: Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Mtambile: Khamis Salum Ali

4. Kusini Unguja
Chwaka: Bhagwanji Meisuria (Mshamba)
Tunguu: Khalifa Salum Suleiman
Uzini: Salum Mwinyi Rehani
Makunduchi: Haji Ameir Haji (Timbe)
Paje: Jaffar Sanya Jussa

5. Magharibi
Dimani: Hafidh Ali Tahir
Fuoni: Abass Ali Hassan
Kiembesamaki: Ibrahim Hassanali Mohamed
Kijitoupele: Shamsi Vuai Nahodha
Mwanakwerekwe: Ahmada Yahya Abdulwakil (Shaa)
Bububu: Mwantakaje Haji Juma
Mfenesini: Col. Mst. Masoud Ali Khamis
Welezo: Saada Mkuya Salum
Mwera: Makame Kassim Makame

6. Mjini
Amani: Mussa Hassan Mussa
Chumbuni: Ussi Salum Pondeza
Magomeni: Jamal Kassim Ali
Mpendae: Salim Hassan Turkey
Shaurimoyo: Matar Ali Salum
Jang’ombe: Ali Hassan Omar (King)
Kikwajuni: Hamad Yussuf Masauni
Kwahani: Dk. Hussein Ali Mwinyi
Malindi: Dkt. Abdulla Juma Abdalla

ORODHA YA MAJIMBO YA UCHAGUZI 2015 BARAZA LA WAWAKILISHI - ZANZIBAR

1. Kaskazini Pemba
Mgogoni: Shehe Hamad Matar
Gando: Maryam Thani Juma
Kojani: Makame Said Juma
Mtambwe: Khadija Omar Kibano
Wete: Harusi Said Suleiman
Micheweni: Shamata Shaame Khamis
Tumbe: Ali Khamis Bakar
Konde: Omar Seif Abeid
Wingwi: Said Omar Said

2. Kaskazini Unguja
Chaani: Nadil Abdul-Latif Jussa
Kijini: Juma Makungu Juma
Mkwajuni: Ussi Yahaya Haji
Nungwi: Ame Haji Ali
Tumbatu: Haji Omar Kheri
Bumbwini: Mtumwa Peya Yussuf
Donge: Dkt. Khalid Salum Mohamed
Kiwengwa: Asha Abdalla Mussaa
Mahonda: Balozi Seif Alli Iddi

3. Kusini Pemba
Chake Chake: Suleiman Sarhan Said
Chonga: Shaibu Said Ali
Ole: Mussa Ali Mussa
Wawi: Hamad Abdalla Rashid
Ziwani: Suleiman Makame Ali

4. Mkoani
Chambani: Bahati Khamis Kombo
Kiwani: Mussa Foum Mussa
Mkoani: Mmanga Mjwengo Mjawiri
Mtambile: Moh’d Mgaza Jecha

5. Kusini Unguja
Chwaka: Issa Haji Ussi
Tunguu: Simai Mohamed Said
Uzini: Mohamedraza H. Dharamsi
Makunduchi: Haroun Ali Suleiman
Paje: Jaku Hashim Ayoub

6. Magharibi
Chukwani: Mwanaasha Khamis Juma
Dimani: Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini
Fuoni: Yussuf Hassan Iddi
Kiembe Samaki: Mahmoud Thabit Kombo
Kijitoupele: Ali Suleiman Ali (Shihata)
Mwanakwerekwe: Abdalla Ali Kombo
Pangawe: Khamis Juma Mwalim
Bububu: Masoud Abraham Masoud
Mfenesini: Machano Othman Said
Mtoni: Hussein Ibrahim Makungu
Mtopepo: Dkt. Makame Alli Ussi
Welezo: Hassan Khamis Hafidh
Mwera: Mihayo Juma N’hunga

6. Mjini
Amani: Rashid Ali Juma
Chumbuni: Miraji Khamis Mussa
Magomeni: Rashid Makame Shamsi
Mpendae: Mohamed Said Mohamed (Dimwa)
Shaurimoyo: Hamza Hassan Juma
Jang’ombe: Abdalla Maulid Diwani
Kikwajuni: Nassor Salum Ali (Jazeera)
Kwahani: Ali Salum Haji
Malindi: Mohamed Ahmada Salum

WABUNGE WA MIKOA WALIOTEULIWA KUPITIA JUMUIYA – UWT

1 Arusha: Catherine Valentine Magige na Vailet Charles Mfuko
2 Dar es Salaam: Mariam Nassoro Kisangi na Janeth Mourice Massaburi
3 Dodoma: Felister Aloyce Bura na Fatuma Hassan Toufiq
4 Geita: Vicky Paschal Kamata na Josephina Tabitha Chagula
5 Iringa: Rose Cyprian Tweve na Ritha Enespher Kabati
6 Katavi: Taska Restuta Mbogo na Anna Richard Lupembe
7 Kagera: Bernadetha Kasabango Mushashu na Oliva Daniel Semuguruka
8 Kigoma: Josephine Johnson Genzabuke na Philipa Geofrey Mturano
9 Kilimanjaro: Shally Josepha Raymond na Betty Eliezer Machangu
10 Lindi: Hamida Mohamed Abdallah na Tecla Mohamed Ungele
11 Mara: Agnes Mathew Wambura na Christina Mwema Samo
12 Manyara: Martha Jachi Umbulla na Esther Alexander Mahawe
13 Mbeya: Dk. Mary Machuche na Mary Obadia Mbwilo
14 Morogoro: Christine Gabriel Ishengoma na Sarah Msafiri Ally
15 Mtwara: Anastazia James Wambura na Agness Elias Hokororo
16 Mwanza: Kemirembe Julius Lwota na Kiteto Zawadi Konshuma
17 Njombe: Dk. Susan Alphonce Kolimba na Neema William Mgaya
18 Pwani: Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu
19 Rukwa: Bupe Nelson Mwakang’ata na Silafu Jumbe Maufi
20 Ruvuma: Jacqueline Ngonyani Msongozi na Sikudhan Yassini Chikambo
21 Simiyu: Esther Lukago Midimu na Leah Jeremia Komanya
Songwe: Juliana Daniel Shonza na Neema Gerald Mwandabila
22 Singida: Aisharose Ndogholi Matembe na Martha Moses Mlata
23 Shinyanga: Lucy Thoma Mayenga na Azza Hillal Hamad
24 Tabora: Munde Tambwe Abdallah na Mwanne Ismail Mchemba
25 Tanga: Ummy Ally Mwalimu na Sharifa O. Abebe

WABUNGE WA MIKOA WALIOTEULIWA KUPITIA JUMUIYA YA UWT - ZANZIBAR
1 Kaskazini Pemba: Maida Hamad Abdalla na Asya Sharif Omar
2 Kaskazini Unguja: Angelina Adam Malembeka na Mwanajuma Kassim Makame
3 Kusini Pemba: Faida Moh’d Bakar na Asha Moh’d Omar
4 Kusini Unguja: Asha Mshimba Jecha na Mwamtum Dau Haji
5 Magharibi: Tauhida Cassian Galos na Kaukab Ali Hassan
6 Mjini Unguja: Fakharia Shomar Khamis na Asha Abdallah Juma

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI – VITI MAALUM – ZANZIBAR
1 Kaskazini Pemba: Bihindi Hamad Khamis na Choum Kombo Khamis
2 Kaskazini Unguja: Panya Ali Abdalla na Mtumwa Suleiman Makame
3 Kusini Pemba: Shadya Moh’d Suleiman na Tatu Moh’d Ussi
4 Kusini Unguja: Salma Mussa Bilali na Wanu Hafidh Ameir
5 Magharibi: Mwanaidi Kassim Mussa na Amina Iddi Mabrouk
6 Mjini: Mgeni Hassan Juma na Saada Ramadhan Mwendwa

WABUNGE WA WALIOTEULIWA KUPITIA MAKUNDI MENGINE
1. Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Halima Abdallah Bulembo
Zainabu Athuman Katimba
Mariamu Dittopile Mzuzuri
Maria Ndilla Kangoye
Sophia Mfaume Kizigo
Irine Uwoya

UVCCM - ZANZIBAR
Khadija Nassir Ali
Munira Mustafa Khatibu
Nadra Juma Mohamed
Time Bakar Sharif

2. Jumuiya ya WAZAZI
Najma Murtaza Giga – (Tanzania Zanzibar)
Zainabu Nuhu Mwamwindi - (Tanzania Bara)

3. Walemavu
Stella Alex Ikupa
Amina Saleh Mollel

4. Vyuo Vikuu
Jasmin Tisekwa Bunga
Esther Michael Mmasi

5. NGO’s
Mchungaji Getrude P. Rwakatare
Khadija Hassan Aboud

6. Wafanyakazi
Angelina Jasmin Kairuki

Hawa Mchafu Chakoma

No comments:

Post a Comment