Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 August 2015

RAIS KIKWETE AAHIDI KUANZISHA TAASISI

Rais Dk. Jakaya Kikwete


Rais Dk. Jakaya Kikwete amesema baada ya kustaafu ataanzisha Taasisi itakayoshugulikia masuala mbalimbali yakiwamo afya ya akina mama na watoto, kilimo, sayansi na teknolojia pamoja na mafunzo ili kuiletea nchi maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa jana Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiwa shahada ya heshima ya Uzamivu  na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Alisema baada ya kumaliza muda wake hataanzisha taasisi ya kushughulikia migogoro bali ataanzisha taasisi itakayokuwa na majukumu ya kusaidia masuala ya akina mama na watoto, kilimo na kuendesha semina na midahalo kwa dhumuni la kuleta maendeleo.
“Nitakapostaafu nataka kuleta taasisi kwa ajili ya kushughulikia wakina mama na watoto, kilimo, midahalo yenye kujenga, nina imani mtasaidia, sitaki taasisi ya  ushauri wa migogoro ila kama itatokea mahala nikaitwa nitaenda kusaidia,” alisema Rais Kikwete.
Aidha, alisema taasisi hiyo itaundwa na wataalamu ambao watakuwa na utaalamu katika masuala ya sayansi na teknolojia, kilimo, afya na midahalo.
Rais Kikwete alisema hatapenda kujishughulisha na masuala ya siasa bali atajikita katika shughuli zake za kilimo cha nanasi na ufugaji.
Alizitaka nchi maskini kukumbatia sayansi na teknolojia kwani bila kufanya hivyo itaziwia vigumu kupiga hatua kimaendeleo.
“Sisi maskini kama hatutakumbatia sayansi na teknolojia hatuwezi kupata maendeleo,” alisema.
Aliongeza kuwa chuo hicho kimejengwa na Serikali pekee ingawa iliomba michango kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof. David Mwakyusa, alisema wamemtunuku rais Kikwete shahada hiyo kwa kutambua mchango wake katika kukuza na uendelezaji wa sayansi na teknolojia na serikali yake kutenga fedha kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment